Skip to main content

Posts

Showing posts from September, 2021

Yanga yazuiwa na CAF kuwatumia AUCHO, DJUMA na FISTON dhidi ya Rivers United

      Zikiwa zimesalia siku chache kuelekea michuano ya CAF kuanza kwa hatua za awali za mtoano, Shirikisho la soka barani Africa CAF limeitaka klabu ya Yanga kutowatumia baadhi ya wachezaji katika mchezo dhidi ya Rivers United. Wachezaji hao ni Khalid Aucho, Fiston Mayele na Djuma Shabani ambao wote ni usajili mpya wa Klabu hiyo. Sababu zinatajwa kuwa ni kucheleweshwa kwa vibali vya wachezaji hao. Adhabu hii inatajwa kuendelea kutumika hata katika mchezo wa pili wa marudiano Utakaochezwa nchini Nigeria. Hata hivyo taarifa kutoka kurugenzi ya habari ya Yanga SC imethibitisha taarifa hizo na kueleza kuwa zuio hilo linatokana na Vilabu walivyokuwa wanacheza wachezaji hao kuchelewesha vibali hivyo. Aidha Uongozi huo umesema kuwa tayari wameshawaandikia barua FIFA kushughulikia sakata hilo kwani wao walikamilisha taratibu zote za usajili mapema isipokuwa vilabu walikotoka ndio walichelewesha kutoa vibali Yanga itawakabili Rivers United siku ya jumapili tarehe 12/9/2021 katika...