Skip to main content

HISTORIA LEO: Siku kama ya leo mwaka jana tarehe 14/4/ 2016

Siku kama ya leo mwaka jana katika michuano ya Europa League, Liverpool ilifunga Borussia Dortmund kwa magoli 4-3katika mchezo ambao hadi kufikia dk. 66 Liverpool ilikuwa ikihitaji jumla ya magoli 3 zaidi ili kuweza kuvuka kwenda hatua ya nusu fainali.
Borrussia Dortmund ambao walishinda katika mchezo wa kwanza kwa ushindi mwembamba wa 2-1, Walikuwa wanakaribishwa katika dimba la Anfield kubabiliana tena na majogoo hao wa London.
Hata hiyo ni haohao Dortmund walioanza kupata magoli mawili ya dakika za mapema kupitia kwa Pierre-Emerick Aubameyang dakika ya 5 kabla ya Henrik Mhkitaryian kuongeza goli la pili dakika ya 9.
Divock Origi aliipatia Liverpool goli la kufutia machozi mapema katika kipindi cha pili dakika ya 48 kabla ya Marco Reus hajaiongezea Dortmund goli la 3 dakika ya 57, lililodumu hadi dakika ya 65.
Kwa idadi hiyo ya magoli iliwafanya Borussia Dortmund kuongoza kwa jumla ya goli 5-2 pamoja na magoli ya mchezo awali.
Liverpool walikuwa na mtihani mkubwa wa kufanya zikiwa zimesalia dakika 25 tu huku wakihitaji magoli 3 kuushangaza ulimwengu wa soka kama walivyowahi kufanya tena 2005 katika fainali za UEFA mjini Istanbul, Uturuki dhidi ya AC Milan.
Alikuwa ni Philippe Coutinho aliyeanzisha matumaini ya kihisia kwa kucheza one-two nzuri na James Milner na kuweka wavuni mpira huku akishangilia kwa kuwaamsha mashabiki wa Liverpool.
Mamadou Sahko alikomesha mpira wavuni mnamo dakika ya 78 kupitia kona iliyochongwa na Coutinho  na kuzidi kuamsha matumaini ya vigogo hao wa uingereza.
Dakika zikielekea kuyoyoma na kiza kikizidi kutanda kwa upande wa liverpool. Beki mkroasia Dejan Lovren akawaduwaza Dortmund kwa kuipatia Liverpool bao la 4 katika mchezo huu kupitia mpira mfupi wa adhabu nje kidogo ya lango la Dortmund ambao Milner aliupiga akitoa pasi kwa Daniel Sturrige aliyekuwa amewatoroka wachezaji wa Dortmund na Sturrige akaingiza krosi iliyopokelewa kwa kichwa na Lovren dakika ya 91.
Kwa matokeo haya Liverpool ikasonga mbele kwa ushindi wa jumla yaani Aggregates wa bao 5-4 dhidi ya Borussia Dortmund na katika hatua ya nusu fainali waliiondosha Villareal ambapo hata hivyo walishindwa kuchukua ubingwa kwa kufungwa na Sevilla FC kwa goli 3-1 mjini Basel, Uswizi
Dejan Lovren wa Liverpool akifunga goli la ushindi dhidi ya Dortmund 

Wachezaji wa Liverpool wakikimbia kushangilia goli la 4 na la Ushindi 
.
  

Comments

Popular posts from this blog

Wajue Wafungaji bora wa EPL kwa kila timu inayoshiriki sasa

1. CHELSEA - Frank Lampard -147 Lampard ndiye anayeshikilia rekodi ya mfungaji bora wa Chelsea wa muda wote yaani tangu (Chelsea) ilipoanzishwa akitupia kambani magoli 211. Alisajiliwa akitokea West ham mwaka 2001 na kwa sasa ni moja kati ya mashujaa wa kubwa wa klabu ya Chelsea. Alifunga goli la kwanza la Premier League akiwa na Chelsea December 23, 2001. Goli la mwisho alilifunga 05 April 2014. 2. TOTTENHAM - Teddy Sheringham - 98 Teddy Sheringham anafahamika kama "Legend" wa Tottenham Hotspurs pamoja na kuvichezea vilabu takribani 10 vya nchini uingereza ikiwemo Manchester United na West ham United. Alisajiliwa na Tottenham akitokea Nottingham Forest mwaka 1992 na alisajiliwa na Man United 1997 kabla ya kurejea tena Tottenham 2001. Aliifungia Spurs goli la kwanza tar.02.september 1992 na la mwisho tar. 21 April 2003 kabla hajatimkia Portsmouth   3. MANCHESTER CITY - Sergio Aguero -120 Akiwa amesaliwa na magoli 10 tu kuwa mfungaji bora wa historia wa M...

Liverpool kuwakumbuka 96 waliokufa janga la Hillsborough: Ifahamu zaidi "HILLSBOROUGH DISASTER"

Familia ya wana Liverpool FC wakiwemo wakiwemo mashabiki, wachezaji, Viongozi wa timu pamoja na wanafamilia na wahanga wa janga la Hillsborough (Hillsborough Family Support Group -HFSG) wataungana leo katika maadhimisho ya kuwakumbuka wapendwa wao waliofariki tarehe kama ya leo miaka 28 iliyopita wakiwa uwanjani. Tukio hilo maarufu kama "HILLSBOROUGH DISASTER 96" lilitokea katika mchezo wa nusu fainali ya mwaka 1988-1989 kati ya Liverpool na Nottingham Forest katika uwanja wa Hillsborough .Katika tukio hili watu 96 walifariki dunia na wengine 766 kujeruhiwa na kuacha kumbukumbu mpaka leo yakuwa ni janga kubwa la kimichezo kuwahi kutokea katika hisporia ya michezo Uingereza. Chanzo cha tukio hili ni amri ya kimakosa ya Afisa polisi ambaye ni mkuu wa siku hiyo Police David Duckenfield iliyoamuru geti la kuingia uwanjani lililojulikana kama Geti "C" kufunguliwa angali nje kulikuwa na idadi kubwa ya mashabiki waliokuwa wakishinikiza kuingia ndani. Baada ya geti hi...

TIMU YA LIGI DARAJA LA KWANZA UINGEREZA YAPANDA DARAJA KWA MARA YA KWANZA

Brighton & Hove Albion imefanikiwa kupanda daraja na hivyo kushiriki ligi kuu ya uingereza msimu ujao baada ya kujikusanyia jumla ya point 79 katika michezo 43 iliyokwisha cheza mpaka sasa ikiwa imesalia michezo 3. Brighton Albion inayonolewa na kocha wa zamani wa Birmingham City na Norwich City, Chris Hughton  itakuwa ni timu ya 48 kushiriki ligi kuu ya uingereza baada ya kupata ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya Wigan Athletics siku ya jumatatu. Kwa upande wake kocha Hughton amesema kuwa anajivunia namna ambavyo timu hiyo walivyojirudi kwa kasi kufuatia hali ya msimu. Aidha ameongeza kuwa kuweka nguvu zao kwa pamoja hadi kufikia hatua hii sio jambo rahisi, na wanahitaji kila aina ya pongezi. Brighton walinusa nafasi ya kucheza ligi kuu ya uingereza msimu uliopita baada ya kuwa katika ushindani mkubwa na kujikuta wakipoteza nafasi hiyo kwa tofauti ya magoli ya kufungwa na kufunga dhidi ya Barnely kufuatia matokeo ya sare waliyoyapata dhidi Middlesbrough. Kufuatia ushindi huu ...