Skip to main content

Arsenal wawalilia Middlesbrough kuwapeleka top 4


  • Calum Chambers apewa kazi ya kufanya. 
  • Lukaku naye ana adhma ya kurejea kwenye mbio za "Golden boot"
Mlinzi wa Arsenal Calum Chambers akimdhibiti Sadio Mane katika 
mechi ya kwanza ya ligi
Kocha wa Middlesbrough Steve Agnew anaamini kuwa wachezaji wa Arsenal wanawasiliana na wachezaji wake katika kuhakikisha wanapata matokeo katika mechi ya mwisho dhidi ya Liverpool ili Arsenal iweze kuipiku Liverpool kubaki nafasi ya nne.

Kocha Steve Agnew amesema kuwa Arsenal imeweka matumaini makubwa kwa mchezaji wao anayeitumikia Middlesbrough kwa mkopo Calum Chambers na wamekuwa wakimtumia jumbe za kumpa ujasiri katika mchezo huo utakaopigwa Anfield.

Arsenal ipo nyuma ya Liverpool kwa alama moja wakijikusanyia alama 73 na liverpool wakiwa na alama 72 huku wote wakisaliwa na mchezo mmoja wa kumalizia ligi hapo kesho. Michezo yote miwili (pamoja mingine yote ya ligi)  itapigwa muda mmoja wakati Liverpool watawakaribisha Middlesbrough na Arsenal watawakaribisha Everton.

Katika hatua nyingine, Arsenal atakuwa na kibarua kizito katika mechi yake dhidi ya Everton na ugumu wa mechi hiyo utachagizwa na Lukaku ambaye atakuwa anahitaji magoli mawili au zaidi ili kubakisha matumaini yake ya kukiwania kiatu cha dhahabu.

Kwasasa Lukaku ana magoli 24 huku Harry Kane akiwa ana magoli 26 baada ya kuonekana mwiba mchingu katika mechi dhidi ya Leicester City alhamis ya juzi, ambapo alifunga magoli manne katika ushindi wa magoli 6-1.
Wakati Everton wakijitahidi kumtengenezea Lukaku nafasi za magoli, Watakuwa pia wakimzuia Sanchez asiongeze magoli kwani naye yupo nyuma ya Lukaku kwa tofauti ya goli 1.
Hali hii inafanya mchezo kati ya Arsenal na Everton pamoja na wa Liverpool na Middlesbrough kuwa na msisimko wa aina yake.

Comments

Popular posts from this blog

Wajue Wafungaji bora wa EPL kwa kila timu inayoshiriki sasa

1. CHELSEA - Frank Lampard -147 Lampard ndiye anayeshikilia rekodi ya mfungaji bora wa Chelsea wa muda wote yaani tangu (Chelsea) ilipoanzishwa akitupia kambani magoli 211. Alisajiliwa akitokea West ham mwaka 2001 na kwa sasa ni moja kati ya mashujaa wa kubwa wa klabu ya Chelsea. Alifunga goli la kwanza la Premier League akiwa na Chelsea December 23, 2001. Goli la mwisho alilifunga 05 April 2014. 2. TOTTENHAM - Teddy Sheringham - 98 Teddy Sheringham anafahamika kama "Legend" wa Tottenham Hotspurs pamoja na kuvichezea vilabu takribani 10 vya nchini uingereza ikiwemo Manchester United na West ham United. Alisajiliwa na Tottenham akitokea Nottingham Forest mwaka 1992 na alisajiliwa na Man United 1997 kabla ya kurejea tena Tottenham 2001. Aliifungia Spurs goli la kwanza tar.02.september 1992 na la mwisho tar. 21 April 2003 kabla hajatimkia Portsmouth   3. MANCHESTER CITY - Sergio Aguero -120 Akiwa amesaliwa na magoli 10 tu kuwa mfungaji bora wa historia wa M...

Liverpool kuwakumbuka 96 waliokufa janga la Hillsborough: Ifahamu zaidi "HILLSBOROUGH DISASTER"

Familia ya wana Liverpool FC wakiwemo wakiwemo mashabiki, wachezaji, Viongozi wa timu pamoja na wanafamilia na wahanga wa janga la Hillsborough (Hillsborough Family Support Group -HFSG) wataungana leo katika maadhimisho ya kuwakumbuka wapendwa wao waliofariki tarehe kama ya leo miaka 28 iliyopita wakiwa uwanjani. Tukio hilo maarufu kama "HILLSBOROUGH DISASTER 96" lilitokea katika mchezo wa nusu fainali ya mwaka 1988-1989 kati ya Liverpool na Nottingham Forest katika uwanja wa Hillsborough .Katika tukio hili watu 96 walifariki dunia na wengine 766 kujeruhiwa na kuacha kumbukumbu mpaka leo yakuwa ni janga kubwa la kimichezo kuwahi kutokea katika hisporia ya michezo Uingereza. Chanzo cha tukio hili ni amri ya kimakosa ya Afisa polisi ambaye ni mkuu wa siku hiyo Police David Duckenfield iliyoamuru geti la kuingia uwanjani lililojulikana kama Geti "C" kufunguliwa angali nje kulikuwa na idadi kubwa ya mashabiki waliokuwa wakishinikiza kuingia ndani. Baada ya geti hi...

TIMU YA LIGI DARAJA LA KWANZA UINGEREZA YAPANDA DARAJA KWA MARA YA KWANZA

Brighton & Hove Albion imefanikiwa kupanda daraja na hivyo kushiriki ligi kuu ya uingereza msimu ujao baada ya kujikusanyia jumla ya point 79 katika michezo 43 iliyokwisha cheza mpaka sasa ikiwa imesalia michezo 3. Brighton Albion inayonolewa na kocha wa zamani wa Birmingham City na Norwich City, Chris Hughton  itakuwa ni timu ya 48 kushiriki ligi kuu ya uingereza baada ya kupata ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya Wigan Athletics siku ya jumatatu. Kwa upande wake kocha Hughton amesema kuwa anajivunia namna ambavyo timu hiyo walivyojirudi kwa kasi kufuatia hali ya msimu. Aidha ameongeza kuwa kuweka nguvu zao kwa pamoja hadi kufikia hatua hii sio jambo rahisi, na wanahitaji kila aina ya pongezi. Brighton walinusa nafasi ya kucheza ligi kuu ya uingereza msimu uliopita baada ya kuwa katika ushindani mkubwa na kujikuta wakipoteza nafasi hiyo kwa tofauti ya magoli ya kufungwa na kufunga dhidi ya Barnely kufuatia matokeo ya sare waliyoyapata dhidi Middlesbrough. Kufuatia ushindi huu ...