Mchezo wa marudiano nusu fainali ya ligi ya mabingwa ulaya kati ya Athletico
Madrid na Real Madrid umemalizika hii leo kwa Athletico Madrid kuchomoza na ushindi wamagoli 2 kwa 1 dhidi ya Real Madrid.
Athletico ndio waliokuwa wa kwanza kupata magoli yote mawili kupitia kwa Saul Niguez dakika ya 13 baada ya kuunganisha kwa kichwa mpira wa kona uliochongwa na Koke.
Athletico walipata goli la 2 kwa njia ya penalt kupitia kwa Antoine
Griezmann baada ya Fernando Torres kufanyiwa madhambi katika eneo la
hatari la madrid.
Mpira uliendelea kwa kasi huku Madrid wakianza kulikaribia lango la Athletico kwa mara nyingi zaidi na
kunako dk ya 43 Isco Alarcon aliipatia Madrid bao la kufuta machozi baada ya shughuli pevu ya Karim Benzema kuwatambuka wachezaji 3 wa Athletico na kutoa pasi kwa Kroos ambaye shuti lake lilipanguliwa na Oblak kabla ya Isco kumalizia.
Mpaka timu zinaenda kwa mapumziko, Athletico 2-1 Madrid.Kipindi cha pili kilianza kwa mpira kuanza kutawaliwa zaidi na wageni Real Madrid ambao licha ya kushindwa kuongeza goli la pili, walifanya mashambulizi ya hatari langoni mwa wapinzani wao ikiwemo mpira uliotiwa nyavuni na Cristiano Ronaldo ambao mwamuzi aliamuru kuwa Ronaldo alikuwa ameshaotea.
Mpaka mwamuzi anapuliza kipenga cha mwisho, Athletico 2-1 Real Madrid. Kufuatia matokeo haya Real Madrid wanatinga fainali na watakutana na Juventus ambao walitangulia hapo jana baada ya kuwaondosha Monaco. Real Madrid atakuwa anatafuta nafasi ya kuutetea ubingwa wake baada ya kulinyakuwa tena kombe hili mwaka jana.
Athletico ndio waliokuwa wa kwanza kupata magoli yote mawili kupitia kwa Saul Niguez dakika ya 13 baada ya kuunganisha kwa kichwa mpira wa kona uliochongwa na Koke.
![]() | |
Saul Niguez akiipatia Athetico Madrid goli la kwanza kwa kichwa |
Mpira uliendelea kwa kasi huku Madrid wakianza kulikaribia lango la Athletico kwa mara nyingi zaidi na
kunako dk ya 43 Isco Alarcon aliipatia Madrid bao la kufuta machozi baada ya shughuli pevu ya Karim Benzema kuwatambuka wachezaji 3 wa Athletico na kutoa pasi kwa Kroos ambaye shuti lake lilipanguliwa na Oblak kabla ya Isco kumalizia.
Mpaka timu zinaenda kwa mapumziko, Athletico 2-1 Madrid.Kipindi cha pili kilianza kwa mpira kuanza kutawaliwa zaidi na wageni Real Madrid ambao licha ya kushindwa kuongeza goli la pili, walifanya mashambulizi ya hatari langoni mwa wapinzani wao ikiwemo mpira uliotiwa nyavuni na Cristiano Ronaldo ambao mwamuzi aliamuru kuwa Ronaldo alikuwa ameshaotea.
Mpaka mwamuzi anapuliza kipenga cha mwisho, Athletico 2-1 Real Madrid. Kufuatia matokeo haya Real Madrid wanatinga fainali na watakutana na Juventus ambao walitangulia hapo jana baada ya kuwaondosha Monaco. Real Madrid atakuwa anatafuta nafasi ya kuutetea ubingwa wake baada ya kulinyakuwa tena kombe hili mwaka jana.
Comments
Post a Comment