
Bale amekuwa akisumbuliwa na majeruhi ya mara kwa mara na amefanikiwa kuanza katika michezo 24 tu msimu huu huku akianza katika michezo 17 tu ya La liga na kupachika jumla ya magoli 9. Hali kwa Bale imekuwa mbaya zaidi pale ambapo wachezaji wanaochukua nafasi yake kama Isco, Marco Asencio na James Rodriguez wakionekana kuitendea haki nafasi hiyo.
Manchester United wapo nafsi ya 5 katika msimamo wa ligi ya EPL huku wakiwa na matumaini machache ya kumaliza katika nafasi ya nne. Hata hivyo matumaini yao yamesalia katika michuano ta Uefa Europa ambapo kwasasa wapo kwenye hatua ya nusu fainali dhidi ya Celta De Vigo na tayari wameshacheza mchezo wa kwanza ambapo Mancheaster United ilitoka kifua mbele ugenini kwa ushindi wa goli 1-0.
Mechi ya marudiano itapigwa Old Trafford kesho jumatano huku kukiwa na kila dalili kuwa Manchester United watafuzu hatua hiyo na wanatabiriwa kukutana na Ajax katika fainali kutokana na matokeo mazuri ya awali Ajax waliyoyapata. Ajax walishinda mchezo wao wa kwanza wakiwa nyumbani Amsterdam kwa magoli 4-1 dhidi ya Lyon. Shukrani za dhati kwa mchezaji wa Chelsea anayekipiga kwa mkopo Ajax Betrand Traore kwa kupachika magoli 2.
Fainali ya kombe la EUROPA itapigwa katika mji wa Stockholm, nchini Sweden.
Na Walter Stephen.
Comments
Post a Comment