Skip to main content

Chelsea Mabingwa Wapya EPL 2016/2017

  • Michy Batchuayi apeleka shangwe kwa wapenzi wa "The Blue". Alazimisha sherehe ianze mapema.
  • Sasa kurejea Stamford Bridge, Watford wakiwapoke kwa makofi kama wafalme
Chelsea wametawazwa rasmi kuwa mabingwa wapya wa Uingereza, England Premier League baada ya kujikusanyia pointi ambazo hakuna timu yoyote kwasasa inayoweza kuzifikia.
Mbelgiji Michy Batchuay ndie aliyelazimisha Chelsea kupewa tiketi ya kuanza kusherekea ubingwa wao baada ya kuipatia chelsea bao pekee dk ya 82 akiteleza kumalizia pasi iliyoingizwa na  Cesar Azpilicueta katika mchezo ulioonekana kuwa mgumu sana.
Batchuayi alitokea benji akichukua nafasi ya Pedro Rodriguez katika mabadiliko mawili ya utata yaliowashangaza mashabiki wa Chelsea ambapo Eden Hazard naye alitolewa na nafasi yake kuchukuliwa na Willian. Baada ya mabadiliko haya Chelsea walianza kushambuliwa lakini ukuta wao ukiongozwa na Cahil, Luiz na Azpilicueta uliweza kuimili vishindo vya wenyeji wao.
Michy Batchuayi akifunga goli 1 na la pekee kwa Chelsea

Ushindi huu umewafanya chelsea mabingwa wa ligi hiyo kwa mara ya 5. Mara ya kwanza walibeba ubingwa msimu wa 2004/2005 chini ya kocha Jose Mourinho, mara ya pili 2005/2006 chini ya Mourinho tena, mara ya tatu 2009/2010 chini ya kocha Carlo Ancelotti, 2014/2015 chini ya Mourinho (baada ya kurejea tena kwa mara ya 2) na sasa 2016/2017 chini ya Antonio Conte.
Wachezaji wa Chelsea wakimrusha juu kocha wao Antonio Conte kuashiria furaha ya ubingwa.
Rekodi zinasemaje:
  • Chelsea wanachukua ubinwa huu kwa mara ya 5.
  • John Terry ndiye mchezaji wa pekee kusherekea mara zote 5 ambazo chelsea amenyakua ubingwa huu.
  • Ushindi huu unamfanya Antonio Conte kuwa kocha wa nne muitaliano kushinda ubingwa wa ligi kuu EPL baada ya Carlo Ancelotti, Roberto Mancini, na Claudio Ranieri.
  • Conte pia anakuwa ni kocha wa 4 kubeba ubingwa huu katika msimu wa kwanza wa makocha na vilabu baada ya kuwahi kufanya hivyo, Jose Mourihno (2004-2005), Carlo Ancelotti (2009-2010) na Manuel Pellegrini (2013-2014)  
Sasa Chelsea watarejea Stamford Bridge kuwakabili Watford huku wakiandandaliwa njia kwa Watford kupanga mistari miwili na wachezaji wa Chelsea kupita katikati huku wakipigiwa makofi na wapinzani mbele ya mashabiki wao nyumbani.
 

Comments

Popular posts from this blog

Wajue Wafungaji bora wa EPL kwa kila timu inayoshiriki sasa

1. CHELSEA - Frank Lampard -147 Lampard ndiye anayeshikilia rekodi ya mfungaji bora wa Chelsea wa muda wote yaani tangu (Chelsea) ilipoanzishwa akitupia kambani magoli 211. Alisajiliwa akitokea West ham mwaka 2001 na kwa sasa ni moja kati ya mashujaa wa kubwa wa klabu ya Chelsea. Alifunga goli la kwanza la Premier League akiwa na Chelsea December 23, 2001. Goli la mwisho alilifunga 05 April 2014. 2. TOTTENHAM - Teddy Sheringham - 98 Teddy Sheringham anafahamika kama "Legend" wa Tottenham Hotspurs pamoja na kuvichezea vilabu takribani 10 vya nchini uingereza ikiwemo Manchester United na West ham United. Alisajiliwa na Tottenham akitokea Nottingham Forest mwaka 1992 na alisajiliwa na Man United 1997 kabla ya kurejea tena Tottenham 2001. Aliifungia Spurs goli la kwanza tar.02.september 1992 na la mwisho tar. 21 April 2003 kabla hajatimkia Portsmouth   3. MANCHESTER CITY - Sergio Aguero -120 Akiwa amesaliwa na magoli 10 tu kuwa mfungaji bora wa historia wa M...

Liverpool kuwakumbuka 96 waliokufa janga la Hillsborough: Ifahamu zaidi "HILLSBOROUGH DISASTER"

Familia ya wana Liverpool FC wakiwemo wakiwemo mashabiki, wachezaji, Viongozi wa timu pamoja na wanafamilia na wahanga wa janga la Hillsborough (Hillsborough Family Support Group -HFSG) wataungana leo katika maadhimisho ya kuwakumbuka wapendwa wao waliofariki tarehe kama ya leo miaka 28 iliyopita wakiwa uwanjani. Tukio hilo maarufu kama "HILLSBOROUGH DISASTER 96" lilitokea katika mchezo wa nusu fainali ya mwaka 1988-1989 kati ya Liverpool na Nottingham Forest katika uwanja wa Hillsborough .Katika tukio hili watu 96 walifariki dunia na wengine 766 kujeruhiwa na kuacha kumbukumbu mpaka leo yakuwa ni janga kubwa la kimichezo kuwahi kutokea katika hisporia ya michezo Uingereza. Chanzo cha tukio hili ni amri ya kimakosa ya Afisa polisi ambaye ni mkuu wa siku hiyo Police David Duckenfield iliyoamuru geti la kuingia uwanjani lililojulikana kama Geti "C" kufunguliwa angali nje kulikuwa na idadi kubwa ya mashabiki waliokuwa wakishinikiza kuingia ndani. Baada ya geti hi...

TIMU YA LIGI DARAJA LA KWANZA UINGEREZA YAPANDA DARAJA KWA MARA YA KWANZA

Brighton & Hove Albion imefanikiwa kupanda daraja na hivyo kushiriki ligi kuu ya uingereza msimu ujao baada ya kujikusanyia jumla ya point 79 katika michezo 43 iliyokwisha cheza mpaka sasa ikiwa imesalia michezo 3. Brighton Albion inayonolewa na kocha wa zamani wa Birmingham City na Norwich City, Chris Hughton  itakuwa ni timu ya 48 kushiriki ligi kuu ya uingereza baada ya kupata ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya Wigan Athletics siku ya jumatatu. Kwa upande wake kocha Hughton amesema kuwa anajivunia namna ambavyo timu hiyo walivyojirudi kwa kasi kufuatia hali ya msimu. Aidha ameongeza kuwa kuweka nguvu zao kwa pamoja hadi kufikia hatua hii sio jambo rahisi, na wanahitaji kila aina ya pongezi. Brighton walinusa nafasi ya kucheza ligi kuu ya uingereza msimu uliopita baada ya kuwa katika ushindani mkubwa na kujikuta wakipoteza nafasi hiyo kwa tofauti ya magoli ya kufungwa na kufunga dhidi ya Barnely kufuatia matokeo ya sare waliyoyapata dhidi Middlesbrough. Kufuatia ushindi huu ...