
Kiungo wa Liverpool Phillippe Coutinho anatarajiwa kurejea katika mchezo dhidi ya Southampton utakaopigwa uwanja wa Anfield kesho jumapili.
Mchezaji huyo amerudi kwenye mazoezi na kujumuika na wenzake, tayari kuwakabili "The Saints".
Coutinho alipata majeruhi katika mchezo dhidi ya Watford mapema wiki hii ambapo alitolewa nje ya uwanja dakika ya 13 na nafasi yake kuchukuliwa na Adam Lallana ambaye naye alikuwa ametoka kuuguza majeruhi.
Katika mchezo huo dhidi ya Watford, Liverpool ilipata ushindi wa goli 1-0 kupitia goli la Emre Can.
Majeruhi ya Coutinho yalizua taharuki miongoni mwa mashabiki wa Liverpool hususani katika kipindi hiki ambapo wanatafuta nafasi ya kushiriki michuano ya ligi ya mabingwa Ulaya msimu ujao huku tayari wakiwa hawana huduma ya Sadio Mane na nahodha wao Jordan Henderson.
Hata hivyo Coutinho mwenyewe amenukuliwa akisema kuwa ni majeruhi madogo na yalimsababishia maumivu kwa siku za mwanzo tu ila kwasasa anaweza kuendelea na mazoezi.
Hapo jana Countinho ameonekana akifanya mazoezi na wachezaji wenzake katika uwanja wa mazoezi wa Melwood kuelekea kuikabili Southampton hapo kesho jumapili.
PICHA: Phillippe Countinho akiwa mazoezini katika viwanja vya Melwood na wenzake
![]() |
Comments
Post a Comment