
Griezmann yuko tayari kukubali kiwango cha paundi 280,000 kwa wiki kama mshahara, na inasemekana Manchester United wako tayari kufikia paundi milioni 89 ambayo ndiyo gharama ya kuuzwa iliyoainishwa kwenye mkataba wake na athletico madrid, kwa mujibu wa jarida la Sun.
Kama habari hizi zitaendelea kuwa njema kwa Manchester United, basi Griezmann atakuwa amenunuliwa kwa dau sawa na Mfaransa mwenzake Paul Pogba ila Griezmann atapokea mshahara mkubwa zaidi.
Kufuatia hatihati hizo za kuondoka Vicente Calderon, tayari kocha wa Athletico Madrid Diego Simeone anamfukuzia kwa karibu Alexis Sanches na Straika wa Olympic Lyon Alexandre Lacazette kama mbadala
Comments
Post a Comment