Skip to main content

Harry Kane ampiku Lukaku mbio za mfungaji bora kwa magoli 2 ndani ya dk 2 za mwisho

Harry Kane jana amejitakatisha kileleni mwa orodha ya wafungaji bora wa EPL baada ya kufunga magoli 4 katika ushindi wa magoli 6 kwa 1 dhidi ya Leicester City.
Kufuatia ushindi huo, Kane sasa anaongoza mbio za kukipata kiatu cha dhahabu kwa kumzidi Lukaku kwa magoli mawili, yeye akiwa na magoli 26 na Lukaku 24.

Kane alifunga goli la kwanza dakika ya 25 akipokea pasi kutoka kwa Heung-Min Son.  Baada ya dakika 11 Heung-Min Son aliipatia Spurs goli la pili akipokea pasi kutoka kwa muingereza Dele Ali.
Leicester City walipata goli la kufutia machozi kipindi cha pili dk ya 59 kupitia kwa mlizi wao Ben Chilwell lakini hata hivyo lilishindwa kuwaongezea munkari wa kubadili matokeo.
Harry Kane alirudi tena kambani kunako dk ya 63 akimalizia jitihada zilizofanywa na Victor Wanyama baada ya mpira wa kichwa uliopigwa kuokolewa na mchezaji wa Leicester.
Kunako dakika ya 71 Heung-Min Son kwa mara nyingine aliiandikia Spurs goli la 4, muda huu Kane akirudisha fadhila kwa Son kwa kutoa pasi ya mwisho.
Tottenham waliendelea kulisakama lango la Leicester kama simba mwenye njaa na zikiwa zimesalia dakika 2 kabla ya kukamilika dakika 90 Harry Kane alitupia goli la 3 na kukamilisha Hat-trick dk 88 akipokea pasi toka kwa Filip Lesniak. Njaa ya kukinyakua kiatu cha dhahabu haikuishia hapo kwa Harry Kane kwani baada muda wa nyongeza kujulikana Kane alikwamisha wavuni goli la nne akipokea pasi kutoka kwa Ben Davies

Comments

Popular posts from this blog

Wajue Wafungaji bora wa EPL kwa kila timu inayoshiriki sasa

1. CHELSEA - Frank Lampard -147 Lampard ndiye anayeshikilia rekodi ya mfungaji bora wa Chelsea wa muda wote yaani tangu (Chelsea) ilipoanzishwa akitupia kambani magoli 211. Alisajiliwa akitokea West ham mwaka 2001 na kwa sasa ni moja kati ya mashujaa wa kubwa wa klabu ya Chelsea. Alifunga goli la kwanza la Premier League akiwa na Chelsea December 23, 2001. Goli la mwisho alilifunga 05 April 2014. 2. TOTTENHAM - Teddy Sheringham - 98 Teddy Sheringham anafahamika kama "Legend" wa Tottenham Hotspurs pamoja na kuvichezea vilabu takribani 10 vya nchini uingereza ikiwemo Manchester United na West ham United. Alisajiliwa na Tottenham akitokea Nottingham Forest mwaka 1992 na alisajiliwa na Man United 1997 kabla ya kurejea tena Tottenham 2001. Aliifungia Spurs goli la kwanza tar.02.september 1992 na la mwisho tar. 21 April 2003 kabla hajatimkia Portsmouth   3. MANCHESTER CITY - Sergio Aguero -120 Akiwa amesaliwa na magoli 10 tu kuwa mfungaji bora wa historia wa M...

Liverpool kuwakumbuka 96 waliokufa janga la Hillsborough: Ifahamu zaidi "HILLSBOROUGH DISASTER"

Familia ya wana Liverpool FC wakiwemo wakiwemo mashabiki, wachezaji, Viongozi wa timu pamoja na wanafamilia na wahanga wa janga la Hillsborough (Hillsborough Family Support Group -HFSG) wataungana leo katika maadhimisho ya kuwakumbuka wapendwa wao waliofariki tarehe kama ya leo miaka 28 iliyopita wakiwa uwanjani. Tukio hilo maarufu kama "HILLSBOROUGH DISASTER 96" lilitokea katika mchezo wa nusu fainali ya mwaka 1988-1989 kati ya Liverpool na Nottingham Forest katika uwanja wa Hillsborough .Katika tukio hili watu 96 walifariki dunia na wengine 766 kujeruhiwa na kuacha kumbukumbu mpaka leo yakuwa ni janga kubwa la kimichezo kuwahi kutokea katika hisporia ya michezo Uingereza. Chanzo cha tukio hili ni amri ya kimakosa ya Afisa polisi ambaye ni mkuu wa siku hiyo Police David Duckenfield iliyoamuru geti la kuingia uwanjani lililojulikana kama Geti "C" kufunguliwa angali nje kulikuwa na idadi kubwa ya mashabiki waliokuwa wakishinikiza kuingia ndani. Baada ya geti hi...

TIMU YA LIGI DARAJA LA KWANZA UINGEREZA YAPANDA DARAJA KWA MARA YA KWANZA

Brighton & Hove Albion imefanikiwa kupanda daraja na hivyo kushiriki ligi kuu ya uingereza msimu ujao baada ya kujikusanyia jumla ya point 79 katika michezo 43 iliyokwisha cheza mpaka sasa ikiwa imesalia michezo 3. Brighton Albion inayonolewa na kocha wa zamani wa Birmingham City na Norwich City, Chris Hughton  itakuwa ni timu ya 48 kushiriki ligi kuu ya uingereza baada ya kupata ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya Wigan Athletics siku ya jumatatu. Kwa upande wake kocha Hughton amesema kuwa anajivunia namna ambavyo timu hiyo walivyojirudi kwa kasi kufuatia hali ya msimu. Aidha ameongeza kuwa kuweka nguvu zao kwa pamoja hadi kufikia hatua hii sio jambo rahisi, na wanahitaji kila aina ya pongezi. Brighton walinusa nafasi ya kucheza ligi kuu ya uingereza msimu uliopita baada ya kuwa katika ushindani mkubwa na kujikuta wakipoteza nafasi hiyo kwa tofauti ya magoli ya kufungwa na kufunga dhidi ya Barnely kufuatia matokeo ya sare waliyoyapata dhidi Middlesbrough. Kufuatia ushindi huu ...