Skip to main content

Manchester united mabingwa wapya Europa 2017


Manchester united chini ya kocha Jose Mourinho imetwaa Kombe la Uefa Europa league baada ya kuilaza Ajax kwa magoli 2-0.
Kwa ushindi huo Manchester inakata tiketi ya kushiriki michuano  ya ligi ya mabingwa ulaya na moja kwa moja wataingia kwenye hatua ya makundi.
Goli la kwanza la Manchester lilifungwa na Paul Pogba dakika ya baada ya kuwekewa mpira na fellaini na kuutenga kabla ya kupiga shuti lililomgusa mlinzi wa Ajax Davinson Sanchez na kumpoteza kipa Andre Onana.
Goli la pili lilifungwa kipindi cha pili kupitia kwa Henrik Mkhitaryan baada ya kuunganisha mpira uliokuwa ukitaka kuokolewa kwa kichwa na mchezaji wa Ajax.
Hata hivyo Ajax ndio waliowaandama Manchester united  licha ya kuonekana wazi kuwa mbinu za kupenya ukuta wa Mashetani hao kugonga mwamba.
Kombe hili linaifanya Manchester united kuwa klabu ya kwanza ya uingereza kuwazidi Liverpool kwa vikombe kwani kwasasa watakuwa na vikombe 42 dhidi ya Liverpool yenye jumla ya vikombe 41.

Comments

Popular posts from this blog

Wajue Wafungaji bora wa EPL kwa kila timu inayoshiriki sasa

1. CHELSEA - Frank Lampard -147 Lampard ndiye anayeshikilia rekodi ya mfungaji bora wa Chelsea wa muda wote yaani tangu (Chelsea) ilipoanzishwa akitupia kambani magoli 211. Alisajiliwa akitokea West ham mwaka 2001 na kwa sasa ni moja kati ya mashujaa wa kubwa wa klabu ya Chelsea. Alifunga goli la kwanza la Premier League akiwa na Chelsea December 23, 2001. Goli la mwisho alilifunga 05 April 2014. 2. TOTTENHAM - Teddy Sheringham - 98 Teddy Sheringham anafahamika kama "Legend" wa Tottenham Hotspurs pamoja na kuvichezea vilabu takribani 10 vya nchini uingereza ikiwemo Manchester United na West ham United. Alisajiliwa na Tottenham akitokea Nottingham Forest mwaka 1992 na alisajiliwa na Man United 1997 kabla ya kurejea tena Tottenham 2001. Aliifungia Spurs goli la kwanza tar.02.september 1992 na la mwisho tar. 21 April 2003 kabla hajatimkia Portsmouth   3. MANCHESTER CITY - Sergio Aguero -120 Akiwa amesaliwa na magoli 10 tu kuwa mfungaji bora wa historia wa M...

Liverpool kuwakumbuka 96 waliokufa janga la Hillsborough: Ifahamu zaidi "HILLSBOROUGH DISASTER"

Familia ya wana Liverpool FC wakiwemo wakiwemo mashabiki, wachezaji, Viongozi wa timu pamoja na wanafamilia na wahanga wa janga la Hillsborough (Hillsborough Family Support Group -HFSG) wataungana leo katika maadhimisho ya kuwakumbuka wapendwa wao waliofariki tarehe kama ya leo miaka 28 iliyopita wakiwa uwanjani. Tukio hilo maarufu kama "HILLSBOROUGH DISASTER 96" lilitokea katika mchezo wa nusu fainali ya mwaka 1988-1989 kati ya Liverpool na Nottingham Forest katika uwanja wa Hillsborough .Katika tukio hili watu 96 walifariki dunia na wengine 766 kujeruhiwa na kuacha kumbukumbu mpaka leo yakuwa ni janga kubwa la kimichezo kuwahi kutokea katika hisporia ya michezo Uingereza. Chanzo cha tukio hili ni amri ya kimakosa ya Afisa polisi ambaye ni mkuu wa siku hiyo Police David Duckenfield iliyoamuru geti la kuingia uwanjani lililojulikana kama Geti "C" kufunguliwa angali nje kulikuwa na idadi kubwa ya mashabiki waliokuwa wakishinikiza kuingia ndani. Baada ya geti hi...

TIMU YA LIGI DARAJA LA KWANZA UINGEREZA YAPANDA DARAJA KWA MARA YA KWANZA

Brighton & Hove Albion imefanikiwa kupanda daraja na hivyo kushiriki ligi kuu ya uingereza msimu ujao baada ya kujikusanyia jumla ya point 79 katika michezo 43 iliyokwisha cheza mpaka sasa ikiwa imesalia michezo 3. Brighton Albion inayonolewa na kocha wa zamani wa Birmingham City na Norwich City, Chris Hughton  itakuwa ni timu ya 48 kushiriki ligi kuu ya uingereza baada ya kupata ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya Wigan Athletics siku ya jumatatu. Kwa upande wake kocha Hughton amesema kuwa anajivunia namna ambavyo timu hiyo walivyojirudi kwa kasi kufuatia hali ya msimu. Aidha ameongeza kuwa kuweka nguvu zao kwa pamoja hadi kufikia hatua hii sio jambo rahisi, na wanahitaji kila aina ya pongezi. Brighton walinusa nafasi ya kucheza ligi kuu ya uingereza msimu uliopita baada ya kuwa katika ushindani mkubwa na kujikuta wakipoteza nafasi hiyo kwa tofauti ya magoli ya kufungwa na kufunga dhidi ya Barnely kufuatia matokeo ya sare waliyoyapata dhidi Middlesbrough. Kufuatia ushindi huu ...