
Kinda wa AS Monaco, Kylian Mbappe (18) amekubali kujiunga na klabu ya Real Madrid ya Hispania akitokea Monaco huku akiwatupilia Mbali Manchester United na PSG iliyokuwa ikimfatilia kwa karibu.
Kwa mujibu wa jarida la Marca la nchini Hispania Mbappe ametoa baraka zake kwa Real Madrid kwenye mchakato wa kutaka atue Bernabeu na tayari maafisa wa Real Madrid wamemkutanisha yeye na familia yake ambao pia ndio wanaomsimamia wake kwenye maswala ya uhamisho.
Taarifa zinasema kuwa Mbappe amekubaliana na uhamishho huo, na msukumo mkubwa ni Kocha wa Real Madrid mfaransa Zinadine Zidane. Hata hivyo ifahamike kuwa Mbappe amekuwa ni mchezaji anayevutiwa sana na staa wa Real Madrid Cristiano Ronaldo na hivyo kuhamia Real Madrid kunatafsiriwa kuwa ni moja ya ndoto ambazo Mbappe angependa kuzitimiza.
Mapema wiki hii Manchester United walitangaza dau kwa mshambuliaji huyo ambalo lilisemekana lingemfanya mchezaji anayelipwa pesa nyingi zaidi klabuni hapo endapo lingekubaliwa. Imetangazwa kuwa Man United waliweka mezani kiasi cha paundi milioni 72 lakini Monaco walitupilia mbali ofa hiyo.
Mbali na Manchester United, Pia PSG walitangaza nia yao ya kumnasa mshambuliaji huyo na mapema mwezi March, The Suns waliripoti kuwa PSG walimwandalia kitita cha paundi millioni 80. Hata hivyo inasemekana kuwa, kama kigezo kingekuwa ni pesa, basi PSG wangekuwa na nafasi nzuri zaidi ya kushinda mbio za kuipata saini ya kinda huyo.
Na Walter Stephen
Comments
Post a Comment