Skip to main content

RONALDO AISULUBU ATHLETICO MADRID KWA HAT-TRICK..

Na walter stephan

Mchezo wa awamu ya kwanza wa nusu fainali ya ligi mabingwa ulaya baina ya Real madrid na Athletico madrid ulimalizika kwa Mchezaji bora wa dunia kwa sasa Cristiano Ronaldo kudhihirisha ubora wake katika michuano hiyo baada ya kufunga magoli yote 3 ambayo timu yake iliyapata.
Mchezo huo ulianza kwa kasi ya kuridhisha na Katika dk ya 7 Carvajal aligongeana pasi vizuri na Isco katika lango la athletico kabla ya kufanya jaribio lililopanguliwa na mlinda mlango Oblak na kumbabatiza benzema ambaye alishindwa kuweka mpira ule kimiani.
Real Madrid ilianza kupata goli la kwanza kupitia kwa Cristiano Ronaldo dk ya 10 baada ya kuunganisha kwa kichwa mpira ulioingizwa eneo la goli la athletico Madrid na carvajal.
Madrid waliendelea kuutawala mpira licha ya nafasi nzuri ya kusawazisha kwa upande wa athletico kupitia kwa Kelvin Gameiro kukataliwa vizuri na mlinda mango wa Real Madrid Kylor Navas.

Katika dk ya 29 benzema aliunganisha Mpira wa tik taka baada ya kazi nzuri ya kuwatambuka mabeki kufanywa na Ronaldo hata hivyo kazi hiyo ya hatari haikuzaa matunda kwa Mpira kupitia sentimita chache juu ya lango la wapinzani wao.
Hadi timu hizo zinaenda mapumziko Real Madrid walikuwa wako mbele kwa goli 1.
Kipindi cha pili kilianza kwa kupooza kiasi huku Athletico wakijaribu kuuweka mpira kwenye himaya yao. Real Madrid iliongeza uhakika wa ushindi dk ya 73 baada ya Ronaldo kuiandikia goli la pili Madrid na goli lake la 102 katika michuano hiyo baada ya kupokea mpira kwa benzema na kupiga shuti Kali lililomshinda mlinda mlango wa athletico Madrid.

Ronaldo akipiga mkwaju na kufunga goli la pili

Ronaldo alikamilisha karamu ya hat-trick kunako dakika ya 86 baada ya kumalizia jitihada kubwa ya Lucas Vazquez aliyerudisha uwanjani Mpira uliokuwa unataka kutoka nje katika lango la watani wao. Hadi kipenga cha mwisho Real  Madrid 3, Athletico Madrid 0.
Ronaldo amekuwa mwiba mkali kwa watani wao wa jadi kwani katika mchezo wa ligi ya Hispania mzunguko wa kwanza, Ronaldo aliwafunga tena Athletico hat-trick na kumfanya awe amewafunga jumla ya magoli sita kwa msimu huu.
Mchezo wa Marudiano utapigwa wiki ijayo siku ya jumatano katika uwanja wa Vicente Calderon katika mji huo huo wa Madrid, wakati huo ambapo Athletico Madrid watakuwa nyumbani.

Comments

Popular posts from this blog

Wajue Wafungaji bora wa EPL kwa kila timu inayoshiriki sasa

1. CHELSEA - Frank Lampard -147 Lampard ndiye anayeshikilia rekodi ya mfungaji bora wa Chelsea wa muda wote yaani tangu (Chelsea) ilipoanzishwa akitupia kambani magoli 211. Alisajiliwa akitokea West ham mwaka 2001 na kwa sasa ni moja kati ya mashujaa wa kubwa wa klabu ya Chelsea. Alifunga goli la kwanza la Premier League akiwa na Chelsea December 23, 2001. Goli la mwisho alilifunga 05 April 2014. 2. TOTTENHAM - Teddy Sheringham - 98 Teddy Sheringham anafahamika kama "Legend" wa Tottenham Hotspurs pamoja na kuvichezea vilabu takribani 10 vya nchini uingereza ikiwemo Manchester United na West ham United. Alisajiliwa na Tottenham akitokea Nottingham Forest mwaka 1992 na alisajiliwa na Man United 1997 kabla ya kurejea tena Tottenham 2001. Aliifungia Spurs goli la kwanza tar.02.september 1992 na la mwisho tar. 21 April 2003 kabla hajatimkia Portsmouth   3. MANCHESTER CITY - Sergio Aguero -120 Akiwa amesaliwa na magoli 10 tu kuwa mfungaji bora wa historia wa M...

Liverpool kuwakumbuka 96 waliokufa janga la Hillsborough: Ifahamu zaidi "HILLSBOROUGH DISASTER"

Familia ya wana Liverpool FC wakiwemo wakiwemo mashabiki, wachezaji, Viongozi wa timu pamoja na wanafamilia na wahanga wa janga la Hillsborough (Hillsborough Family Support Group -HFSG) wataungana leo katika maadhimisho ya kuwakumbuka wapendwa wao waliofariki tarehe kama ya leo miaka 28 iliyopita wakiwa uwanjani. Tukio hilo maarufu kama "HILLSBOROUGH DISASTER 96" lilitokea katika mchezo wa nusu fainali ya mwaka 1988-1989 kati ya Liverpool na Nottingham Forest katika uwanja wa Hillsborough .Katika tukio hili watu 96 walifariki dunia na wengine 766 kujeruhiwa na kuacha kumbukumbu mpaka leo yakuwa ni janga kubwa la kimichezo kuwahi kutokea katika hisporia ya michezo Uingereza. Chanzo cha tukio hili ni amri ya kimakosa ya Afisa polisi ambaye ni mkuu wa siku hiyo Police David Duckenfield iliyoamuru geti la kuingia uwanjani lililojulikana kama Geti "C" kufunguliwa angali nje kulikuwa na idadi kubwa ya mashabiki waliokuwa wakishinikiza kuingia ndani. Baada ya geti hi...

TIMU YA LIGI DARAJA LA KWANZA UINGEREZA YAPANDA DARAJA KWA MARA YA KWANZA

Brighton & Hove Albion imefanikiwa kupanda daraja na hivyo kushiriki ligi kuu ya uingereza msimu ujao baada ya kujikusanyia jumla ya point 79 katika michezo 43 iliyokwisha cheza mpaka sasa ikiwa imesalia michezo 3. Brighton Albion inayonolewa na kocha wa zamani wa Birmingham City na Norwich City, Chris Hughton  itakuwa ni timu ya 48 kushiriki ligi kuu ya uingereza baada ya kupata ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya Wigan Athletics siku ya jumatatu. Kwa upande wake kocha Hughton amesema kuwa anajivunia namna ambavyo timu hiyo walivyojirudi kwa kasi kufuatia hali ya msimu. Aidha ameongeza kuwa kuweka nguvu zao kwa pamoja hadi kufikia hatua hii sio jambo rahisi, na wanahitaji kila aina ya pongezi. Brighton walinusa nafasi ya kucheza ligi kuu ya uingereza msimu uliopita baada ya kuwa katika ushindani mkubwa na kujikuta wakipoteza nafasi hiyo kwa tofauti ya magoli ya kufungwa na kufunga dhidi ya Barnely kufuatia matokeo ya sare waliyoyapata dhidi Middlesbrough. Kufuatia ushindi huu ...