Skip to main content

Sagna, Navas, Clichy na Caballero waonyeshwa mlango wa kutokea Man City

Klabu ya Manchester City imethibitisha kuachana na wachezaji wake 5 wakiwemo Jesus Navas, Gael Clichy, Bacary Sagna, Pablo Zabaleta na Willy Caballero.
Wachezaji hao mikataba yao inaisha msimu huu na klabu haiko tayari kuwaongezea mkataba mpya.
Tofauti na wengine, Zabaleta alithibitishwa mapema wiki hii kua angeondoka City huku wengine wakijua hatima yao leo hii.
Clichy alijiunga na Manchester City mwaka 2011 akitokea Arsenal na amebeba makombe manne akiwa na Manchester City ikiwemo la ligi kuu 2012 na 2014 na Kombe la ligi mwaka 2014 na 2016.
Navas aliyesajiliwa mwaka 2014 alifanikiwa kubeba makombe matatu yakiwemo hayo mawili ya Kombe la ligi na la ligi kuu 2014.Tayari klabu ya Valencia wameonyesha nia ya kumsajili mhispania huyo.
 Kwa upande wa Zabaleta ambaye yeye na Kompany ndio wachezaji waliokaa Man City kwa muda mrefu kwa wachezaji waliopo mpaka sasa, naye anaondoka huku klabu ya West Ham wakiwa njiani kukamilisha usajili wa kumpokea mkongwe huyo muda wowote.
Pablo alisajiliwa akitokea klabu ya Espanyol ya nchini Hispania mwaka 2008 na mpaka sasa ameichezea City jumla ya mechi 230 za ligi kuu pekee ukiachia michuano mingine.
Caballero yeye alisajiliwa na City mwaka 2014 na alikuwa langoni katika fainali ya Kombe la ligi dhidi ya Liverpool 2016 ambapo wakuwa mabingwa. Amekuwa akihudumia kama mlinzi wa akiba wa Man City kutokana na ubora wa kipa namba moja Joe Hart ambaye baada ya ujio wa Guardiola alitolewa kwa mkopo kwenda Torino.
Ujio wa Guardiola uliambatana na ujio wa mlinda lango wa Barcelona Claudio Bravo ila makosa ya kipa huyo langoni ambaye alikuwa chaguo la kwanza la Pep Guardiola mwanzo mwa msimu, yalimfanya Caballero kufurahia muda zaidi langoni kipindi cha ungwe ya pili ya ligi kuu msimu huu. Mlinzi huyo anaachana na City angali akiwa kwenye jitihada za kuomba kusalia klabuni hapo.
Naye beki wa kulia wa timu hiyo Bacary Sagna amethibitishwa kuondoka klabuni hapo akiwa ameitumikia kwa misimu mitatu tu. Sagna alisajiliwa majira ya joto mwezi July 2014 akitokea Arsenal na ameichezea City jumla ya mechi 85.
Kwa upande wa Yaya Toure ambaye alizungumziwa kuachana na klabu hiyo, hali inaonekana huenda akaendelea kuitumikia. Habari ambazo hazijathibitishwa na klabu yake ni kwamba Toure amepewa tena mkataba wa mwaka mmoja wa kuitumikia. 
Kati ya wachezaji sita (6) wa City waliozungumziwa kuondoka kutokana na mikataba yao kuisha mwisho mwa msimu huu, Toure atakuwa mchezaji pekee aliye bahatika kusalia endapo ni kweli amesaini mkataba huo.

Comments

Popular posts from this blog

Wajue Wafungaji bora wa EPL kwa kila timu inayoshiriki sasa

1. CHELSEA - Frank Lampard -147 Lampard ndiye anayeshikilia rekodi ya mfungaji bora wa Chelsea wa muda wote yaani tangu (Chelsea) ilipoanzishwa akitupia kambani magoli 211. Alisajiliwa akitokea West ham mwaka 2001 na kwa sasa ni moja kati ya mashujaa wa kubwa wa klabu ya Chelsea. Alifunga goli la kwanza la Premier League akiwa na Chelsea December 23, 2001. Goli la mwisho alilifunga 05 April 2014. 2. TOTTENHAM - Teddy Sheringham - 98 Teddy Sheringham anafahamika kama "Legend" wa Tottenham Hotspurs pamoja na kuvichezea vilabu takribani 10 vya nchini uingereza ikiwemo Manchester United na West ham United. Alisajiliwa na Tottenham akitokea Nottingham Forest mwaka 1992 na alisajiliwa na Man United 1997 kabla ya kurejea tena Tottenham 2001. Aliifungia Spurs goli la kwanza tar.02.september 1992 na la mwisho tar. 21 April 2003 kabla hajatimkia Portsmouth   3. MANCHESTER CITY - Sergio Aguero -120 Akiwa amesaliwa na magoli 10 tu kuwa mfungaji bora wa historia wa M...

Liverpool kuwakumbuka 96 waliokufa janga la Hillsborough: Ifahamu zaidi "HILLSBOROUGH DISASTER"

Familia ya wana Liverpool FC wakiwemo wakiwemo mashabiki, wachezaji, Viongozi wa timu pamoja na wanafamilia na wahanga wa janga la Hillsborough (Hillsborough Family Support Group -HFSG) wataungana leo katika maadhimisho ya kuwakumbuka wapendwa wao waliofariki tarehe kama ya leo miaka 28 iliyopita wakiwa uwanjani. Tukio hilo maarufu kama "HILLSBOROUGH DISASTER 96" lilitokea katika mchezo wa nusu fainali ya mwaka 1988-1989 kati ya Liverpool na Nottingham Forest katika uwanja wa Hillsborough .Katika tukio hili watu 96 walifariki dunia na wengine 766 kujeruhiwa na kuacha kumbukumbu mpaka leo yakuwa ni janga kubwa la kimichezo kuwahi kutokea katika hisporia ya michezo Uingereza. Chanzo cha tukio hili ni amri ya kimakosa ya Afisa polisi ambaye ni mkuu wa siku hiyo Police David Duckenfield iliyoamuru geti la kuingia uwanjani lililojulikana kama Geti "C" kufunguliwa angali nje kulikuwa na idadi kubwa ya mashabiki waliokuwa wakishinikiza kuingia ndani. Baada ya geti hi...

TIMU YA LIGI DARAJA LA KWANZA UINGEREZA YAPANDA DARAJA KWA MARA YA KWANZA

Brighton & Hove Albion imefanikiwa kupanda daraja na hivyo kushiriki ligi kuu ya uingereza msimu ujao baada ya kujikusanyia jumla ya point 79 katika michezo 43 iliyokwisha cheza mpaka sasa ikiwa imesalia michezo 3. Brighton Albion inayonolewa na kocha wa zamani wa Birmingham City na Norwich City, Chris Hughton  itakuwa ni timu ya 48 kushiriki ligi kuu ya uingereza baada ya kupata ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya Wigan Athletics siku ya jumatatu. Kwa upande wake kocha Hughton amesema kuwa anajivunia namna ambavyo timu hiyo walivyojirudi kwa kasi kufuatia hali ya msimu. Aidha ameongeza kuwa kuweka nguvu zao kwa pamoja hadi kufikia hatua hii sio jambo rahisi, na wanahitaji kila aina ya pongezi. Brighton walinusa nafasi ya kucheza ligi kuu ya uingereza msimu uliopita baada ya kuwa katika ushindani mkubwa na kujikuta wakipoteza nafasi hiyo kwa tofauti ya magoli ya kufungwa na kufunga dhidi ya Barnely kufuatia matokeo ya sare waliyoyapata dhidi Middlesbrough. Kufuatia ushindi huu ...