Golden State Worriors wameiadhibu kwa mara ya tatu mfululizo Cleveland Caverliers katika fainali ya tatu iliyopigwa alfajiri ya kuamkia leo kwa pointi 118 - 113.
Katika mchezo huo ambao Caverliers walionekana kubadilika tofauti na fainali mbili za nyuma, walijikuta wakiangukia tena pua katika dakika za mwisho na kupoteza mchezo huo.
Worriors walikuwa nyuma ya Cavs katika muda mwingi wa mchezo huo ambao Cavs waliongoza hadi robo ya mwisho kwakuwa mbele kwa point 6 lakini katika dakika 3:09 za mwisho Cavs walishindwa kufunga point yeyote huku Worriors wakibadili matokeo na kufanya mchezo huo kuisha kwa matokeo hayo.
![]() | ||||||
Mshambuliji wa Cleveland Caverliers LeBron James akurusha mpira kuwapita Kelvin Durrant na Zaza Pachilia wa Golden State Worriors katika mchezo wa fainali ya 3 |
![]() |
Mshambuliaji wa GSW Kelvin Durrant akupasua katikati ya Tristan Thomson na JR Smith wa Caverliers katika mechi ya fainali ya 3 |
Comments
Post a Comment