Kiungo mahiri wa timu ya taifa ya Ivory Coast ambaye pia ameitumikia klabu ya Newcastle United Cheick Tiote amefariki dunia akiwa kwenye mazoezi na timu yake ya Beijing Enterprises ya nchini china.
Tiote aliyezoeleka kucheza nafasi ya kiungo mkabaji amefariki dunia ghafla jioni hii majira ya saa 12, bila kuonyesha na dalili zozote za ugonjwa baada ya kuanguka chini na kuzimia uwanjani.
Mchezaji huyo alikimbizwa hospitalini lakini alifariki dunia takribani saa moja baadae huku bado ikiwa haijafahamika ni nini kimepelekea mauti yake.
Wakala wa mchezaji huyo Emanuele Palladino pamoja timu hiyo wamethibisha kutokea kwa kifo hicho na tayari familia ya Tiote.
Tiote amefariki akiwa na umri wa miaka 30 na aliitumikia Anderletch ya ubelgiji kati ya 2005 - 2008 kabla ya kuhamia FC Twente 2008 na kuitumikia hadi 2010. Baada ya hapo alisajiliwa na Newcastle na aliitumikia mpaka mapema mwaka huu 2017 alipojiunga na Beijing Enterprises ya china mwezi Februari.

Comments
Post a Comment