Skip to main content

Chelsea yaanza mbio za kumrejesha Lukaku Stanford Bridge

Chelsea imeanzisha mazungumzo na klabu ya Everton yakutaka kumrejesha mshambuliaji wao wa zamani Romelu Lukaku (23) pale Stanford Bridge, kwa mujibu wa The Times.
Lukaku ambaye klabu yake ya Everton imesema anathamani ya Paundi milioni 100 anatakuwa na Chelsea ili kuziba pengo la Diego Costa ambaye hatima yake ya kusalia katika kikosi cha Antonio Conte bado haijafahamika.
Hata hivyo inaaminika kuwa Chelsea hawako tayari kutoa kiwango hicho cha fedha kwa Lukaku ila watakuwa tayari kutoa kiwango kidogo zaidi pamoja na kuwapatia mshambuliaji wao Michy Batchuayi.
Kwa upande wake Batchuayi ameonyesha kutotaka kwenda Goodson Park na badala yake anatamani kujiunga na mabingwa wa Ufaransa, AS Monaco.
Wiki hii Lukaku amenukuliwa akisema kuwa, hatarajii kubakia na Everton msimu ujao na kuongeza kuwa wakala wake Mino Raiola anazungumza na timu nyingine.
Lukaku aliwahi kuitumikia Chelsea akisajiliwa kutoka Anderlecht 2011 ambapo aliichezea Chelsea mechi 10 tu za ligi bila kufunga goli. Baadae Chelsea ilimtoa kwa mkopo kwenda West Bromwich akicheza msimu mmoja wa 2012/2013 na kuweka kambani magoli 17, huku akiifunga hat-trick katika mechi ya mwisho dhidi ya Manchester United katika mchezo wa kumuaga kocha Alex Ferguson.
Romelu Lukaku akipokea maelekezo kutoka kwa kocha wake wa zamani Jose Mourinho
Msimu uliofuata alitolewa tena kwa mkopo kwenda Everton ambako alifunga magoli 15 katika ligi na Everton ikaingia makubaliano na Chelsea ya Jose Mourinho, na kumnunua mshambuliaji huyo wa Ubelgiji mwaka 2014.


Comments

Popular posts from this blog

Wajue Wafungaji bora wa EPL kwa kila timu inayoshiriki sasa

1. CHELSEA - Frank Lampard -147 Lampard ndiye anayeshikilia rekodi ya mfungaji bora wa Chelsea wa muda wote yaani tangu (Chelsea) ilipoanzishwa akitupia kambani magoli 211. Alisajiliwa akitokea West ham mwaka 2001 na kwa sasa ni moja kati ya mashujaa wa kubwa wa klabu ya Chelsea. Alifunga goli la kwanza la Premier League akiwa na Chelsea December 23, 2001. Goli la mwisho alilifunga 05 April 2014. 2. TOTTENHAM - Teddy Sheringham - 98 Teddy Sheringham anafahamika kama "Legend" wa Tottenham Hotspurs pamoja na kuvichezea vilabu takribani 10 vya nchini uingereza ikiwemo Manchester United na West ham United. Alisajiliwa na Tottenham akitokea Nottingham Forest mwaka 1992 na alisajiliwa na Man United 1997 kabla ya kurejea tena Tottenham 2001. Aliifungia Spurs goli la kwanza tar.02.september 1992 na la mwisho tar. 21 April 2003 kabla hajatimkia Portsmouth   3. MANCHESTER CITY - Sergio Aguero -120 Akiwa amesaliwa na magoli 10 tu kuwa mfungaji bora wa historia wa M...

Liverpool kuwakumbuka 96 waliokufa janga la Hillsborough: Ifahamu zaidi "HILLSBOROUGH DISASTER"

Familia ya wana Liverpool FC wakiwemo wakiwemo mashabiki, wachezaji, Viongozi wa timu pamoja na wanafamilia na wahanga wa janga la Hillsborough (Hillsborough Family Support Group -HFSG) wataungana leo katika maadhimisho ya kuwakumbuka wapendwa wao waliofariki tarehe kama ya leo miaka 28 iliyopita wakiwa uwanjani. Tukio hilo maarufu kama "HILLSBOROUGH DISASTER 96" lilitokea katika mchezo wa nusu fainali ya mwaka 1988-1989 kati ya Liverpool na Nottingham Forest katika uwanja wa Hillsborough .Katika tukio hili watu 96 walifariki dunia na wengine 766 kujeruhiwa na kuacha kumbukumbu mpaka leo yakuwa ni janga kubwa la kimichezo kuwahi kutokea katika hisporia ya michezo Uingereza. Chanzo cha tukio hili ni amri ya kimakosa ya Afisa polisi ambaye ni mkuu wa siku hiyo Police David Duckenfield iliyoamuru geti la kuingia uwanjani lililojulikana kama Geti "C" kufunguliwa angali nje kulikuwa na idadi kubwa ya mashabiki waliokuwa wakishinikiza kuingia ndani. Baada ya geti hi...

TIMU YA LIGI DARAJA LA KWANZA UINGEREZA YAPANDA DARAJA KWA MARA YA KWANZA

Brighton & Hove Albion imefanikiwa kupanda daraja na hivyo kushiriki ligi kuu ya uingereza msimu ujao baada ya kujikusanyia jumla ya point 79 katika michezo 43 iliyokwisha cheza mpaka sasa ikiwa imesalia michezo 3. Brighton Albion inayonolewa na kocha wa zamani wa Birmingham City na Norwich City, Chris Hughton  itakuwa ni timu ya 48 kushiriki ligi kuu ya uingereza baada ya kupata ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya Wigan Athletics siku ya jumatatu. Kwa upande wake kocha Hughton amesema kuwa anajivunia namna ambavyo timu hiyo walivyojirudi kwa kasi kufuatia hali ya msimu. Aidha ameongeza kuwa kuweka nguvu zao kwa pamoja hadi kufikia hatua hii sio jambo rahisi, na wanahitaji kila aina ya pongezi. Brighton walinusa nafasi ya kucheza ligi kuu ya uingereza msimu uliopita baada ya kuwa katika ushindani mkubwa na kujikuta wakipoteza nafasi hiyo kwa tofauti ya magoli ya kufungwa na kufunga dhidi ya Barnely kufuatia matokeo ya sare waliyoyapata dhidi Middlesbrough. Kufuatia ushindi huu ...