Ligi ya kikapu nchini marekani maarufu kama NBA imemalizika hii leo kwa timu ya Goldern State Warriors kubeba ubingwa mbele ya wapinzani wao Cleveland Caverliers kwa alama 4-1.
Katika fainali hiyo ambayo ilikuwa ni ya 5, Warriors wamepata ushindi wa pointi 129 dhidi ya 120 za Caverliers na kutawazwa kuwa mabingwa wapya wa NBA kwa msimu wa 2016/2017.
Ushindi huu unahitimishwa kwa fainali 5 tu kati ya 7 zilizopangwa kutokana na Warriors kuwa mbele kwa michezo 4 dhidi ya Cavs walioshinda mchezo 1 jambo linalowafanya Warriors wasiweze tena kufikiwa na Cavs hata kama wangepoteza michezo miwili iliyosalia.
Staa wa Goldern State Warriors Kelvin Durrant, ametajwa kuwa mchezaji bora wa fainali za mwaka huu 2017 za NBA (NBA final MVP Player 2017) ikiwa ni msimu wake wa kwanza kuichezea Warriors baada ya kusajiliwa mwezi June 2016 akitokea Oklahoma City Thunders
Durrant ameonekana kustahili tuzo hiyo baada ya kutoa mchango mkubwa zaidi kwa Warriors katika ubingwa huu, kwa kufunga pointi zaidi ya 30 katika fainali zote 5. Durrant amefunga pointi 38, 33, 31, 35 na 39 katika fainali ya NBA mwaka huu.
PICHA ZA MATUKIO YA FAINALI YA NBA 2017
 |
Staa wa Cavs LeBron James akipamuacha Durrant na kupachika mpira kwenye kikapu |
 |
Andre Iguodala wa Goldern State Warriors aki-dunk na kufunga dhidi ya Cavs |
 |
Stephen Curry akishangilia na mwanae baada ya ushindi |
 |
Kelvin Durrant wa Goldern State Warriors akishangilia mbele ya Kyrie Irving Caverliers |
Comments
Post a Comment