
Griezmann ameweka wazi kuwa sasa ni rasmi atabakia Athletico Madrid kuitumikia na kuondosha tetesi kuwa angejiunga na Manchester United msimu huu.
Kupitia ukurasa wake Twitter, Mfaransa huyo mwenye umri wa miaka 26 ameandika maneno kwa lugha ya kihispania yaliyosomeka "Ahora más que nunca #Atleti #Todosjuntos" yaani akimaanisha "Sasa zaidi ya Milele Atletico tupopamoja".
Hapo jana tarehe 1 June, kupitia ukurasa wetu huu wa Rada Yetu Sports, iliripotiwa habari ya kukataliwa kwa rufaa ya Atletico Madrid, waliyokuwa wameiwasilisha kwenye mahakama ya usuluishi wa masuala ya kimichezo (Court of Attribution of Sports - CAS) iliyolenga kupinga katazo walilopewa na FIFA la kufanya usajili wa wachezaji msimu huu.
Hata hivyo rufaa hiyo ilitupiliwa mbali na CAS na hivyo kuwafanya Atletico kuendelea kutumiki a adhabu hiyo.
Hali hii ilishusha matumaini kwa mashabiki wa Manchester United waliokuwa wanashauku ya kumuona Griezmann akitua Trafford kwani ilishahisiwa na wengi kuwa kufuatia kukataliwa kwa rufaa hiyo, uongozi wa Atletico ungeanza jitiada za kumshawishi Griezmann kubaki katika kikosi hicho cha Diego Simeoni.
![]() |
Alichoposti Griezmann kwenye ukurasa wake wa twitter |
Comments
Post a Comment