Klabu ya Liverpool imethibitisha kuachana na mbio za kumajili beki wa Southampton Mholazi Virgil Van Dijk kufuatia kutoelewana na klabu yake ya Southampton.
Liverpool imekuwa ikiwania saini ya beki huyo, ikishindana na Manchester City na Chelsea ikiwa ni malengo ya kocha Jurgen Klopp kuimarisha kikosi cha Liverpool kunachotarajiwa kucheza michuano ya Ulaya endapo watafuzu kwenye mechi za mtoano.
Hapo jana Southampton ilitishia kuishitaki Liverpool kwenye bodi ya Premier League ikiwatuhumu kutofuata utaratibu katika kumshawishi mchezaji huyo. Hayo yakejiri ikiwa ni muda mchache baada ya Van Dijk kukata mzizi wa fitna kuwa angependa kujiunga na kocha Klopp pale Anfield.
Kupitia tovuti yao, Liverpool wameweka wazi kuwa hawatomuwania tena mchezaji huyo na wanawaomba radhi Southampton.
"Tunapenda kuwaomba radhi wamiliki, bodi ya wakurugenzi pamoja na mashabiki wa Southampton kwa sintofahamu iliyojitokeza katika kumuwania Van Dijk.Tunaiheshimu nafasi ya Southampton na tunathibitisha sasa kuacha kumuwania mchezaji huyo" Ilisomeka taarifa hiyo ya Liverpool.
Liverpool wanarudisha nyuma mikono yao, wakati ambao mashabiki wa Liverpool wikuwa wakifurahia taarifa ya mchezaji huyo kuichagua timu yao na tayari kulikuwa na kila dalili kuwa mchezaji huyo angehamia Anfield.

Comments
Post a Comment