Real Madrid wamechukua tena ubingwa wa ligi ya mabingwa ulaya UEFA kwa mara ya pili mfululizo baada ya kuigaragaza Juventus kwa mabao 4-1.
Madrid wanavunja rekodi ya kuchua kombe hilo mara mbili mfululizo tangu michuano hiyo ilipoanza kutambulika kama michuano ya ligi ya mabingwa Ulaya yaani Uefa champions league.
Mchezo ulianza kwa kasi iliyoashiria Juventus huenda wangeutawala mchezo zaidi kwani walikuwa wakifika langoni kwa Madrid mara kwa mara.
Madrid walikuwa wa kwanza kupata goli kupitia kwa Cristiano Ronaldo dk ya 20 kabla ya Mario Mandzuckic kuisawazishia Juventus. Kipindi cha kwanza kiliisha kwa timu kwenda sare ya goli 1-1.
Kipindi cha pili kilianza kwa Real Madrid kuja tofauti na mnamo dk.61 tu Kiungo mbrazil Casemiro aliunganisha shuti kuelekea langoni mwa Juventus na kuguswa na beki hivyo kumshinda mlinda mlango Buffon.
Ronaldo aliiandikia Madrid goli la 3 baada ya kazi nzuri ya Luka modric.
Kocha zidane alifanya mabadiliko katika kikosi cha madrid kwa kumtoa Benzema na kumuingiza Gareth Bale na baadae kumtoa Isco na kumuingia Marco Asensio.
Mabadiliko hayo yalizaa matunda kwani kunako dk.89 Marco Asensio aliifungia Madrid goli la 4 akipokea pasi ya Marcelo aliyewatambuka vizuri walinzi wa Juventus.
Hata hivyo Juventus walilazimika kucheza pungufu dk 10 za mwisho baada ya Guadrado aliyeingia dk 66 kupata kadi ya manjano dk 72 na kadi ya nyekundu dk 77 baada ya kuonyeshwa kadi ya pili ya njano.

Comments
Post a Comment