Skip to main content

Manchester United na Morata wakubaliana

Manchester United na Staa wa Real Madrid Alvaro Morata wamekubaliana juu ya kuhamia katika kikosi hicho cha Jose Mourinho.
Mazungumzo yamesalia tu kati ya klabu hizo mbili kuona kama ofa ya Manchester itaafikiwa na Real Madrid, rasmi kwa staa huyo kutimka Bernabeu. 
Morata ambaye alikuwa na shauku ya kukihama kikosi cha Real Madrid kutokana na kukosa namba ya kudumu, amefikia hatua nzuri na Manchester huku Los Blancos wakimthaminisha Morata kufikia dau la paundi milioni 78.
Alvaro Morata ambaye ni zao la familia hiyo ya Madrid almaarufu Los Blancos aliwahi kuihama Madrid mwaka 2014 na kutimkia Juventus ambako aliitumikia kwa miaka 2 kabla ya kurejeshwa tena katika kikosi hicho kwa Euro milioni 30 mwezi June 2016.
Ofa ya awali ya Manchester United kwa mshambuliaji huyo iliyofikia paundi milioni 52 ilikataliwa na Madrid na sasa Mashetani hao wekundu wameonyesha nia ya kusajili mchezaji huyo kwakuongeza ofa hiyo.
Mpaka sasa Manchester United imeweka mezani ofa ya Paundi milioni 65 na huenda wakaafikiana na Madrid kwani tetesi zinasema kuwa huenda Manchester wakatangaza kukamilisha usajili huo wiki ijayo.
Morata ameanza katika mechi 19 ambazo Real Madrid imeshuka dimbani chini ya kocha Zinadine Zidane huku Karim Benzema akipewa nafasi zaidi dhidi yake.


Comments

Popular posts from this blog

Wajue Wafungaji bora wa EPL kwa kila timu inayoshiriki sasa

1. CHELSEA - Frank Lampard -147 Lampard ndiye anayeshikilia rekodi ya mfungaji bora wa Chelsea wa muda wote yaani tangu (Chelsea) ilipoanzishwa akitupia kambani magoli 211. Alisajiliwa akitokea West ham mwaka 2001 na kwa sasa ni moja kati ya mashujaa wa kubwa wa klabu ya Chelsea. Alifunga goli la kwanza la Premier League akiwa na Chelsea December 23, 2001. Goli la mwisho alilifunga 05 April 2014. 2. TOTTENHAM - Teddy Sheringham - 98 Teddy Sheringham anafahamika kama "Legend" wa Tottenham Hotspurs pamoja na kuvichezea vilabu takribani 10 vya nchini uingereza ikiwemo Manchester United na West ham United. Alisajiliwa na Tottenham akitokea Nottingham Forest mwaka 1992 na alisajiliwa na Man United 1997 kabla ya kurejea tena Tottenham 2001. Aliifungia Spurs goli la kwanza tar.02.september 1992 na la mwisho tar. 21 April 2003 kabla hajatimkia Portsmouth   3. MANCHESTER CITY - Sergio Aguero -120 Akiwa amesaliwa na magoli 10 tu kuwa mfungaji bora wa historia wa M...

Liverpool kuwakumbuka 96 waliokufa janga la Hillsborough: Ifahamu zaidi "HILLSBOROUGH DISASTER"

Familia ya wana Liverpool FC wakiwemo wakiwemo mashabiki, wachezaji, Viongozi wa timu pamoja na wanafamilia na wahanga wa janga la Hillsborough (Hillsborough Family Support Group -HFSG) wataungana leo katika maadhimisho ya kuwakumbuka wapendwa wao waliofariki tarehe kama ya leo miaka 28 iliyopita wakiwa uwanjani. Tukio hilo maarufu kama "HILLSBOROUGH DISASTER 96" lilitokea katika mchezo wa nusu fainali ya mwaka 1988-1989 kati ya Liverpool na Nottingham Forest katika uwanja wa Hillsborough .Katika tukio hili watu 96 walifariki dunia na wengine 766 kujeruhiwa na kuacha kumbukumbu mpaka leo yakuwa ni janga kubwa la kimichezo kuwahi kutokea katika hisporia ya michezo Uingereza. Chanzo cha tukio hili ni amri ya kimakosa ya Afisa polisi ambaye ni mkuu wa siku hiyo Police David Duckenfield iliyoamuru geti la kuingia uwanjani lililojulikana kama Geti "C" kufunguliwa angali nje kulikuwa na idadi kubwa ya mashabiki waliokuwa wakishinikiza kuingia ndani. Baada ya geti hi...

TIMU YA LIGI DARAJA LA KWANZA UINGEREZA YAPANDA DARAJA KWA MARA YA KWANZA

Brighton & Hove Albion imefanikiwa kupanda daraja na hivyo kushiriki ligi kuu ya uingereza msimu ujao baada ya kujikusanyia jumla ya point 79 katika michezo 43 iliyokwisha cheza mpaka sasa ikiwa imesalia michezo 3. Brighton Albion inayonolewa na kocha wa zamani wa Birmingham City na Norwich City, Chris Hughton  itakuwa ni timu ya 48 kushiriki ligi kuu ya uingereza baada ya kupata ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya Wigan Athletics siku ya jumatatu. Kwa upande wake kocha Hughton amesema kuwa anajivunia namna ambavyo timu hiyo walivyojirudi kwa kasi kufuatia hali ya msimu. Aidha ameongeza kuwa kuweka nguvu zao kwa pamoja hadi kufikia hatua hii sio jambo rahisi, na wanahitaji kila aina ya pongezi. Brighton walinusa nafasi ya kucheza ligi kuu ya uingereza msimu uliopita baada ya kuwa katika ushindani mkubwa na kujikuta wakipoteza nafasi hiyo kwa tofauti ya magoli ya kufungwa na kufunga dhidi ya Barnely kufuatia matokeo ya sare waliyoyapata dhidi Middlesbrough. Kufuatia ushindi huu ...