Kocha wa zamani wa Manchester City Roberto Mancini amesaini mkataba na Miamba ya Urusi Zenit St. Petersburg kwaaji ya kuanza kukinoa kikosi hicho.
Mancini amekaa bila timu ya kuifundisha tangu mwezi wa nane mwaka jana (2016) baada ya kutimuliwa na klabu aliyokuwa akiifundisha ya Inter Milan.
Zenit wamekuwa na mwenendo mbaya wa kisoka kwa miaka miwili mfululizo hali iliyopelekea kutimuliwa kwa kocha Mircea Lucescu (71)
Zenit imemaliza msimu katika nafasi ya tatu, nyuma ya Spartak Moscow ambao ndio mabingwa wapya na CSKA Moscow walioshika nafasi ya pili.
Kufuatia kushika nafasi hiyo, Zenit watashindwa kushiriki michuano ya ligi ya mabingwa ulaya kwa msimu ujao.
Baada ya kuondoka Manchester City 2013, Mancini amekuwa kocha wa Galatasalary ya Uturuki na Inter Milan ya Italia na hivyo kumfanya awe amefundisha timu tatu tofauti kwa kipindi cha miaka 3.

Comments
Post a Comment