Athletico Madrid walikata rufaa hiyo kufuatia adhabu waliyopewa mwezi Julai 2016 na shirikisho la soka duniani FIFA ya kutosajili mchezaji mpya kwa madirisha mawili ya usajili yaani Januari 2017 na Julai 2017 mwaka huu pamoja na kulipa faini ya Paundi 719,793.
Adhabu hii walipewa kufuatia kuvunja sheria za FIFA zinazohusu usajili kwa wachezaji wenye umri wa chini ya miaka 18.
Athletico Madrid aliadhibiwa kipindi kimoja na mahasimu wao Real Madrid kwa makosa yanayofanana ila rufaa ya Real Madrid iliyowasilishwa kwa CAS mwaka jana ilikubaliwa mwezi Desemba 2016 kwa kupunguziwa adhabu ya kutosajili kwa kipindi cha dirisha dogo la Januari tu.
Hali hiyo iliwafanya Real Madrid kutumikia adhabu yao kwa mwezi wa Januari na hivyo kuruhusiwa kuendelea na usajili wa wachezaji wapya katika kipindi hiki cha usajili (July 2017)
Pamoja na kukataliwa kwa rufaa ya Athletico madrid, wamepunguziwa adhabu ya faini waliyotakiwa kulipa kutoka Paundi. 719,793 hadi paundi 439,873.
Kufuatia taarifa hii Athletico Madrid itaathirika kwenye mbio za kumsajili mshambuliaji wa Ufaransa na timu ya Lyon, Alexandre Lacazette ambaye tangu awali aliweka wazi kuwa Athletico Madrid ndiyo sehemu anayodhani kuwa ni sahihi kuendelezea soka lake na tayari miamba hiyo kutoka Vicente Calderon walishaanza mbio za kumuwania.
Taarifa hii pia huenda ikawa mbaya kwa kocha Jose Mourinho na klabu ya Manchester United waliokuwa wakimuhitaji mshambuliaji wa Athletico Madrid, Antoine Griezmann kwani huenda Athletico wakaanza mazungumzo ya kumuomba asiondoke ingawa makubaliano ya mkataba yalikuwa yanamruhusu Griezmann kuondoka msimu huu.
Taarifa hii pia huenda ikawa njema kwa Liverpool waliokuwa wakiwania saini la Lacazzette ingawa Arsenal pia imeingia katika mbio hizo hasa baada ya kutoka kwa taarifa hii.
Comments
Post a Comment