Ripoti zinasema kuwa Tottenham Hotspurs wanakaribia kufikia makubaliano ya kumuuza beki wao wa kulia Kyle Walker kwa ada inayodaiwa kufikia paundi milioni 40.
Pep Guardiola amekuwa akiwania saini ya mchezaji huyo tangu kumalizika kwa msimu ulioisha wa 2016/2017.
Inadaiwa pia kuwa Walker anataka kuondoka Totenham kufuatia viashiria vya kukosa namba dhidi ya Kieran Trippier aliyekuwa akipewa nafasi zaidi katika wiki za mwisho za msimu uliopita.
Guardiola anataka kuimarisha kikosi chake kufuatia kuwapunguza baadhi ya wachezaji wake hasa katika eneo la ulinzi. Tayari kocha huyo ameshaachana na Backary Sagna pamoja na Pablo Zabaleta ambao wote walikuwa wanacheza katika nafasi hiyo.
Zabaleta ameshajiunga na wagonga nyundo wa London West Ham United huku Backary Sagna akiwaniwa kwa karibu na Rafael Benitez aliyepanda daraja na kikosi cha Newcastle United.
Walker mwenye umri wa miaka 27 alitua White Hart Lane mwaka 2009 akitokea Sheffield United ambapo hata hivyo aliendelea kutoa huduma nje ya Spurs kwa mkopo akizichezea QPR, Aston Villa na Sheffield yenyewe kabla ya kuanza kuaminiwa rasmi na Spurs.

Comments
Post a Comment