Skip to main content

Oxlade Chamberlain agoma kuongeza mkataba Arsenal

Kiungo wa Arsenal na timu ya taifa ya Uingereza Oxlade Chamberlain amegoma kuongeza muda wa kusalia katika kikosi hicho cha washika bunduki wa London.
Mkataba wa Chamberlain unafikia ukomo mwaka 2018 hivyo umesalia mwaka mmoja tu na tayari ameonekana kutokuwa tayari kusalia Arsenal.
Taarifa hizi huenda zisiwashitue wengi kufuatia mara kadhaa staa huyo kudai kuwa hafuraishwi na muda anaopewa kushuka dimbani, na zaidi akidai kuchezeshwa katika nafasi asiyoitaka. Chamberlain amekuwa akitumika katika nafasi ya kiungo mshambuliaji, akitokea winga ya kulia (mara nyingine kushoto) wakati yeye anapendelea zaidi kuwa kiungo wa kati.
Huenda habari zikawa zimechagizwa zaidi na taarifa za kutakiwa na kocha wa Liverpool Jurgen Klopp ambaye inadaiwa Liverpool wako tayari kumsajili ila wakitegemea Arsenal kupunguza dau la mchezaji huyo kutoka kwenye kiwango cha paundi milioni 25 ambacho wanakihitaji (Asenal).
Habari hii huenda ikawa mbaya kimaslahi kwa Arsenal kwani Chamberlain akisalia katika kikosi hicho bila kusaini mkataba mpya, atakuwa mchezaji huru mwakani na hivyo kuondoka bure bila kuifaidisha Arsenal.
Yamkini Liverpool nao wanauona ugumu huu unaowakabili Arsenal na ndio maana hawako tayari kutoa kiwango wanachotaka Arsenal kwani wanaamini kwa kuhofia kumpoteza kama mchezaji huru mwakani, basi watakuwa tayari kumuuza hata chini ya paundi milioni 20 kuliko kuja kumuacha aondoke bure hapo baadae.
Mara kadhaa Chamberlain amenukuliwa akisema anapenda kucheza nafasi ya kiungo wa kati huku akimtaja Steven Gerrard kama mtu ambaye angependa kuwa kama yeye.

Na Walter S. Lyakurwa

NYINGINEZO:

Comments

Popular posts from this blog

Wajue Wafungaji bora wa EPL kwa kila timu inayoshiriki sasa

1. CHELSEA - Frank Lampard -147 Lampard ndiye anayeshikilia rekodi ya mfungaji bora wa Chelsea wa muda wote yaani tangu (Chelsea) ilipoanzishwa akitupia kambani magoli 211. Alisajiliwa akitokea West ham mwaka 2001 na kwa sasa ni moja kati ya mashujaa wa kubwa wa klabu ya Chelsea. Alifunga goli la kwanza la Premier League akiwa na Chelsea December 23, 2001. Goli la mwisho alilifunga 05 April 2014. 2. TOTTENHAM - Teddy Sheringham - 98 Teddy Sheringham anafahamika kama "Legend" wa Tottenham Hotspurs pamoja na kuvichezea vilabu takribani 10 vya nchini uingereza ikiwemo Manchester United na West ham United. Alisajiliwa na Tottenham akitokea Nottingham Forest mwaka 1992 na alisajiliwa na Man United 1997 kabla ya kurejea tena Tottenham 2001. Aliifungia Spurs goli la kwanza tar.02.september 1992 na la mwisho tar. 21 April 2003 kabla hajatimkia Portsmouth   3. MANCHESTER CITY - Sergio Aguero -120 Akiwa amesaliwa na magoli 10 tu kuwa mfungaji bora wa historia wa M...

Liverpool kuwakumbuka 96 waliokufa janga la Hillsborough: Ifahamu zaidi "HILLSBOROUGH DISASTER"

Familia ya wana Liverpool FC wakiwemo wakiwemo mashabiki, wachezaji, Viongozi wa timu pamoja na wanafamilia na wahanga wa janga la Hillsborough (Hillsborough Family Support Group -HFSG) wataungana leo katika maadhimisho ya kuwakumbuka wapendwa wao waliofariki tarehe kama ya leo miaka 28 iliyopita wakiwa uwanjani. Tukio hilo maarufu kama "HILLSBOROUGH DISASTER 96" lilitokea katika mchezo wa nusu fainali ya mwaka 1988-1989 kati ya Liverpool na Nottingham Forest katika uwanja wa Hillsborough .Katika tukio hili watu 96 walifariki dunia na wengine 766 kujeruhiwa na kuacha kumbukumbu mpaka leo yakuwa ni janga kubwa la kimichezo kuwahi kutokea katika hisporia ya michezo Uingereza. Chanzo cha tukio hili ni amri ya kimakosa ya Afisa polisi ambaye ni mkuu wa siku hiyo Police David Duckenfield iliyoamuru geti la kuingia uwanjani lililojulikana kama Geti "C" kufunguliwa angali nje kulikuwa na idadi kubwa ya mashabiki waliokuwa wakishinikiza kuingia ndani. Baada ya geti hi...

TIMU YA LIGI DARAJA LA KWANZA UINGEREZA YAPANDA DARAJA KWA MARA YA KWANZA

Brighton & Hove Albion imefanikiwa kupanda daraja na hivyo kushiriki ligi kuu ya uingereza msimu ujao baada ya kujikusanyia jumla ya point 79 katika michezo 43 iliyokwisha cheza mpaka sasa ikiwa imesalia michezo 3. Brighton Albion inayonolewa na kocha wa zamani wa Birmingham City na Norwich City, Chris Hughton  itakuwa ni timu ya 48 kushiriki ligi kuu ya uingereza baada ya kupata ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya Wigan Athletics siku ya jumatatu. Kwa upande wake kocha Hughton amesema kuwa anajivunia namna ambavyo timu hiyo walivyojirudi kwa kasi kufuatia hali ya msimu. Aidha ameongeza kuwa kuweka nguvu zao kwa pamoja hadi kufikia hatua hii sio jambo rahisi, na wanahitaji kila aina ya pongezi. Brighton walinusa nafasi ya kucheza ligi kuu ya uingereza msimu uliopita baada ya kuwa katika ushindani mkubwa na kujikuta wakipoteza nafasi hiyo kwa tofauti ya magoli ya kufungwa na kufunga dhidi ya Barnely kufuatia matokeo ya sare waliyoyapata dhidi Middlesbrough. Kufuatia ushindi huu ...