![]() |
Rooney akiichezea Everton kwenye mchezo wa heshima kwa mmoja wa mashujaa wa klabu hiyo Duncan Ferguson mwaka 2015 |
Rooney mwenye umri wa miaka 31 sasa anarejea Everton ikiwa ni miaka 13 sasa tangu alipoiacha na kutimkia Manchester United mwaka 2004 nha anatarajiwa kusaini mkataba wa miaka miwili
Akiwa bado kinda katika klabu ya Everton, Rooney aliifungia magoli 17 katika michezo 77 aliyocheza, ambayo ilijumuisha misimu miwili ya kuitumikia klabu hiyo ya Merseyside.
Wakati uhamisho wa Rooney ukiwa katika hatua za mwisho, Manchester United nao wapo katika hatua za mwisho za kumtangaza Romelu Lukaku aliyetoka Everton kuwa mchezaji wao mpya.
Mshambuliaji huyo ameposti picha kwenye ukurasa wake wa Instagram akionyesha matukio mbali mbali wakati akifanyiwa vipimo.
Rooney atakuwa ni mshambuliaji wa pili kuondoka United baada ya Msweden Zlatan Ibrahmovic kuachiwa huru mwezi uliopita.
Comments
Post a Comment