Skip to main content

Yanga yazuiwa na CAF kuwatumia AUCHO, DJUMA na FISTON dhidi ya Rivers United

 

 

 

Zikiwa zimesalia siku chache kuelekea michuano ya CAF kuanza kwa hatua za awali za mtoano, Shirikisho la soka barani Africa CAF limeitaka klabu ya Yanga kutowatumia baadhi ya wachezaji katika mchezo dhidi ya Rivers United.

Wachezaji hao ni Khalid Aucho, Fiston Mayele na Djuma Shabani ambao wote ni usajili mpya wa Klabu hiyo. Sababu zinatajwa kuwa ni kucheleweshwa kwa vibali vya wachezaji hao. Adhabu hii inatajwa kuendelea kutumika hata katika mchezo wa pili wa marudiano Utakaochezwa nchini Nigeria.

Hata hivyo taarifa kutoka kurugenzi ya habari ya Yanga SC imethibitisha taarifa hizo na kueleza kuwa zuio hilo linatokana na Vilabu walivyokuwa wanacheza wachezaji hao kuchelewesha vibali hivyo.

Aidha Uongozi huo umesema kuwa tayari wameshawaandikia barua FIFA kushughulikia sakata hilo kwani wao walikamilisha taratibu zote za usajili mapema isipokuwa vilabu walikotoka ndio walichelewesha kutoa vibali

Yanga itawakabili Rivers United siku ya jumapili tarehe 12/9/2021 katika kutafuta tiketi ya kuingia hatua ya makundi ya michuano ya Klabu bingwa Afrika.

Comments

Popular posts from this blog

Wajue Wafungaji bora wa EPL kwa kila timu inayoshiriki sasa

1. CHELSEA - Frank Lampard -147 Lampard ndiye anayeshikilia rekodi ya mfungaji bora wa Chelsea wa muda wote yaani tangu (Chelsea) ilipoanzishwa akitupia kambani magoli 211. Alisajiliwa akitokea West ham mwaka 2001 na kwa sasa ni moja kati ya mashujaa wa kubwa wa klabu ya Chelsea. Alifunga goli la kwanza la Premier League akiwa na Chelsea December 23, 2001. Goli la mwisho alilifunga 05 April 2014. 2. TOTTENHAM - Teddy Sheringham - 98 Teddy Sheringham anafahamika kama "Legend" wa Tottenham Hotspurs pamoja na kuvichezea vilabu takribani 10 vya nchini uingereza ikiwemo Manchester United na West ham United. Alisajiliwa na Tottenham akitokea Nottingham Forest mwaka 1992 na alisajiliwa na Man United 1997 kabla ya kurejea tena Tottenham 2001. Aliifungia Spurs goli la kwanza tar.02.september 1992 na la mwisho tar. 21 April 2003 kabla hajatimkia Portsmouth   3. MANCHESTER CITY - Sergio Aguero -120 Akiwa amesaliwa na magoli 10 tu kuwa mfungaji bora wa historia wa M...

Liverpool kuwakumbuka 96 waliokufa janga la Hillsborough: Ifahamu zaidi "HILLSBOROUGH DISASTER"

Familia ya wana Liverpool FC wakiwemo wakiwemo mashabiki, wachezaji, Viongozi wa timu pamoja na wanafamilia na wahanga wa janga la Hillsborough (Hillsborough Family Support Group -HFSG) wataungana leo katika maadhimisho ya kuwakumbuka wapendwa wao waliofariki tarehe kama ya leo miaka 28 iliyopita wakiwa uwanjani. Tukio hilo maarufu kama "HILLSBOROUGH DISASTER 96" lilitokea katika mchezo wa nusu fainali ya mwaka 1988-1989 kati ya Liverpool na Nottingham Forest katika uwanja wa Hillsborough .Katika tukio hili watu 96 walifariki dunia na wengine 766 kujeruhiwa na kuacha kumbukumbu mpaka leo yakuwa ni janga kubwa la kimichezo kuwahi kutokea katika hisporia ya michezo Uingereza. Chanzo cha tukio hili ni amri ya kimakosa ya Afisa polisi ambaye ni mkuu wa siku hiyo Police David Duckenfield iliyoamuru geti la kuingia uwanjani lililojulikana kama Geti "C" kufunguliwa angali nje kulikuwa na idadi kubwa ya mashabiki waliokuwa wakishinikiza kuingia ndani. Baada ya geti hi...

TIMU YA LIGI DARAJA LA KWANZA UINGEREZA YAPANDA DARAJA KWA MARA YA KWANZA

Brighton & Hove Albion imefanikiwa kupanda daraja na hivyo kushiriki ligi kuu ya uingereza msimu ujao baada ya kujikusanyia jumla ya point 79 katika michezo 43 iliyokwisha cheza mpaka sasa ikiwa imesalia michezo 3. Brighton Albion inayonolewa na kocha wa zamani wa Birmingham City na Norwich City, Chris Hughton  itakuwa ni timu ya 48 kushiriki ligi kuu ya uingereza baada ya kupata ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya Wigan Athletics siku ya jumatatu. Kwa upande wake kocha Hughton amesema kuwa anajivunia namna ambavyo timu hiyo walivyojirudi kwa kasi kufuatia hali ya msimu. Aidha ameongeza kuwa kuweka nguvu zao kwa pamoja hadi kufikia hatua hii sio jambo rahisi, na wanahitaji kila aina ya pongezi. Brighton walinusa nafasi ya kucheza ligi kuu ya uingereza msimu uliopita baada ya kuwa katika ushindani mkubwa na kujikuta wakipoteza nafasi hiyo kwa tofauti ya magoli ya kufungwa na kufunga dhidi ya Barnely kufuatia matokeo ya sare waliyoyapata dhidi Middlesbrough. Kufuatia ushindi huu ...