- Michy Batchuayi apeleka shangwe kwa wapenzi wa "The Blue". Alazimisha sherehe ianze mapema.
- Sasa kurejea Stamford Bridge, Watford wakiwapoke kwa makofi kama wafalme.
Mbelgiji Michy Batchuay ndie aliyelazimisha Chelsea kupewa tiketi ya kuanza kusherekea ubingwa wao baada ya kuipatia chelsea bao pekee dk ya 82 akiteleza kumalizia pasi iliyoingizwa na Cesar Azpilicueta katika mchezo ulioonekana kuwa mgumu sana.
Batchuayi alitokea benji akichukua nafasi ya Pedro Rodriguez katika mabadiliko mawili ya utata yaliowashangaza mashabiki wa Chelsea ambapo Eden Hazard naye alitolewa na nafasi yake kuchukuliwa na Willian. Baada ya mabadiliko haya Chelsea walianza kushambuliwa lakini ukuta wao ukiongozwa na Cahil, Luiz na Azpilicueta uliweza kuimili vishindo vya wenyeji wao.
Michy Batchuayi akifunga goli 1 na la pekee kwa Chelsea |
Ushindi huu umewafanya chelsea mabingwa wa ligi hiyo kwa mara ya 5. Mara ya kwanza walibeba ubingwa msimu wa 2004/2005 chini ya kocha Jose Mourinho, mara ya pili 2005/2006 chini ya Mourinho tena, mara ya tatu 2009/2010 chini ya kocha Carlo Ancelotti, 2014/2015 chini ya Mourinho (baada ya kurejea tena kwa mara ya 2) na sasa 2016/2017 chini ya Antonio Conte.
Wachezaji wa Chelsea wakimrusha juu kocha wao Antonio Conte kuashiria furaha ya ubingwa. |
- Chelsea wanachukua ubinwa huu kwa mara ya 5.
- John Terry ndiye mchezaji wa pekee kusherekea mara zote 5 ambazo chelsea amenyakua ubingwa huu.
- Ushindi huu unamfanya Antonio Conte kuwa kocha wa nne muitaliano kushinda ubingwa wa ligi kuu EPL baada ya Carlo Ancelotti, Roberto Mancini, na Claudio Ranieri.
- Conte pia anakuwa ni kocha wa 4 kubeba ubingwa huu katika msimu wa kwanza wa makocha na vilabu baada ya kuwahi kufanya hivyo, Jose Mourihno (2004-2005), Carlo Ancelotti (2009-2010) na Manuel Pellegrini (2013-2014)
Comments
Post a Comment