Skip to main content

Wajue Wafungaji bora wa EPL kwa kila timu inayoshiriki sasa

1. CHELSEA - Frank Lampard -147
Lampard ndiye anayeshikilia rekodi ya mfungaji bora wa Chelsea wa muda wote yaani tangu (Chelsea) ilipoanzishwa akitupia kambani magoli 211. Alisajiliwa akitokea West ham mwaka 2001 na kwa sasa ni moja kati ya mashujaa wa kubwa wa klabu ya Chelsea. Alifunga goli la kwanza la Premier League akiwa na Chelsea December 23, 2001. Goli la mwisho alilifunga 05 April 2014.


2. TOTTENHAM - Teddy Sheringham - 98
Teddy Sheringham anafahamika kama "Legend" wa Tottenham Hotspurs pamoja na kuvichezea vilabu takribani 10 vya nchini uingereza ikiwemo Manchester United na West ham United. Alisajiliwa na Tottenham akitokea Nottingham Forest mwaka 1992 na alisajiliwa na Man United 1997 kabla ya kurejea tena Tottenham 2001. Aliifungia Spurs goli la kwanza tar.02.september 1992 na la mwisho tar. 21 April 2003 kabla hajatimkia Portsmouth
 


3. MANCHESTER CITY - Sergio Aguero -120
Akiwa amesaliwa na magoli 10 tu kuwa mfungaji bora wa historia wa Manchester City, Aguero anashikilia rekodi ya mfungaji bora wa Premier League wa Man City kwa jumla ya magoli 120. Kun Aguero alisajiliwa kutoka Athletico Madrid July 2011na goli lake la kwanza la ligi alifunga tar 15 August 2011na la mwisho amefunga 29 April 2017 dhidi ya Middlesbrough.


4. LIVERPOOL - Robbie Fowler - 128
Fowler ni mmoja kati ya mashujaa wa Liverpool akiwa ameifungia klabu hiyo magoli 183 huku 128 yakiwa ni ya ligi kuu. Aliitumikia Liverpool kati ya mwaka 1993 hadi 2001, kabla ya kuhamia Leeds na baadae Manchester City kisha alirejea tena Liverpool 2006-2007.Alistaafu soka akiwa na klabu ya Muangthong United ya Thailand mwaka 2012 na sasa anaendesha vipindi katika televisheni ya Liverpool (LFCTV)

5. ARSENAL - Thiery Henry - 175
Henry ndiye "legendary" namba 1 wa Arsenal akiwa ameipachikia jumla ya magoli 228 huku ya ligi yakiwa 175. Goli lake la kwanza alilifunga  18 Sep 1999 na la mwisho 11 Feb 2012 aliporejea kwa mkopo kutoka New York Red Bulls, klabu aliyoitumikia akitokea Barcelona na kustaafu hapo hapo mwaka 2014. Kwasasa Henry ni mchambuzi wa soka huku akitumaini kuitumikia Arsenal kama mkufunzi hapo baadae.


6. MANCHESTER UNITED - Wayne Rooney - 183
Akivunja rekodi mapema mwaka huu ya kuwa mfungaji bora wa historia wa Manchester United, rekodi iliyokuwa ikishikiliwa na shujaa namba 1 wa Manchester United Sir Bobby Chalton, Rooney ndiye anayeshikilia rekodi ya kufunga magoli mengi ya EPL kwa Manchester.Goli  la kwanza alilifunga tar.24 Oct 2004 na la mwisho alilifunga juzi tar 14 May 2017 dhidi  ya Tottenham.

7. EVERTON - Romelu Lukaku - 67
Lukaku ndiye mshambuliaji mwenye mafanikio zaidi katika klabu ya Everton kwa miaka ya karibuni. Lukaku alisajiliwa na Everton akitokea Chelsea ambako alishindwa kuonyesha cheche kwenye lango la wapinzani.
Akiwa Everton ameitumikia kwa mafanikio, hususani msimu huu ambapo mpaka sasa ndiye anayeongoza kwa ufungaji katika EPL. Lukaku alifunga goli la kwanza na Everton tar.21 sep 2013 na goli la mwisho tar.15 April 2017.

 8. SOUTHAMPTON - Matt Le Tissier - 101
Matt ni mmoja wa wachezaji waliochezea Southampton kwa muda mrefu na kucheza michezo mingi pia. Akitokea timu ya vijana hapo hapo Southampton alijumuishwa na kucheza timu ya wakubwa kuanzia 1986 - 2002 akifanikiwa kucheza mechi 443 na kufunga magoli 161 huku 101 yakiwa ya ligi kuu. Goli la kwanza alilifunga tar. 19 August 1992 na la mwisho tar. 19 May 2001.


9. WEST BROMWICH ALBION - Peter Odemwingie - 30
Mnigeria huyu kwasasa ana umri wa miaka 35 akichezea klabu ya Madura United. Odemwingie ameifungia West Bromwich goli la kwanza tar. 21 August 2010 baada ya kusajiliwa akitokea Lokomotiv Moscow na goli la mwisho alifunga tar.19 Jan 2013.

 10. AFC BOURNEMOUTH - Joshua King - 22
Bournemouth wameshiriki Premier League kwa mara ya kwanza mwaka 2015. Akiwa na umri wa miaka 25 tu anaongoza horodha ya wafungaji bora wa magoli katika ligi hiyo. King alifunga goli la kwanza tar.21 Nov 2015 na goli la mwisho alifunga juzi tar.13 May 2017.

11. LEICESTER CITY - Jammie Vardy - 41
Pengine nyota yeke ilichelewa kung'ara lakini nani anasema umri ndio unaocheza mpira muda wote? La hasha, bali hutegemea na mtu kama alivyowahi kuniukuliwa Zlatan Ibrahomovic. Akiwa na umri wa miaka 29 ndipo alikuwa na mafanikio, zaidi ya hapo kabla. Alikuwa shujaa kwa wanafamilia wa Leicester City msimu uliopita kwa kuisaidia kunyakuwa taji la ligi kuu ya Uingereza kwa mara ya kwanza. Aliifungia Leicester goli la kwanza tar.21 Sep 2014 na goli la mwisho tar.29 Apr 2017.


12.WEST HAM UNITED - Paolo Di Canio - 48
Di Canio (mzee wa kupiga Saluti) ni muitalia na amechezea vilabu vingi na vikubwa vya serie A ikiwemo Juventus, AC Milan, Napoli, Lazio na Ternana kabla hajahamia Uingereza mwaka 1997 akiwa na vilabu vingine lakini kujiunga na West Ham ilikuwa mwaka 1999. Aliichezea West Ham mechi 118 za ligi na kufunga magoli 48. Goli la kwanza alifunga tar.27 Feb 1999 na la mwisho tar.11 May 2003


13. CRYSTAL PALACE - Chris Armstrong - 23
 Armstong ameitumikia Palace kwa takribani miaka 3 tu na ndiye anayeongoza kuifungia magoli mengi pamoja na kuitumikia zaidi Tottenham kwa miaka takribani 7. Aliifungia Palace goli la kwanza tar.12 Sep 1992 na mara ya mwisho kufunga ilikuwa tar. 14 May 1995 na baada ya hapo alitimkia Tottenham na kisha Bolton Wanderers.




 14. STOKE CITY - Jonathan Walters - 43
Mpaka sasa anakipiga katika klabu ya Stoke City akiwa na umri wa miaka 33 na ameanza kuitumikia Stoke tangu mwaka 2010 akiletwa na kocha Tony Pulis ambaye kwa sasa anaifundisha West Brom. Goli la kwanza la Walters alifunga tar.02 Oct 2010 na la mwisho tar.08 Apr 2017
15. BURNLEY - Danny Ings - 12
Danny Ings ambaye kwasasa anaitumikia Liverpool huku majeruhi yakimpoteza kabisa kwenye uwanja, ndiye anayeongoza kwa ufungaji wa magoli ya ligi kwa Barnley . Pengine idadi ya magoli 12 inaweza kuonekana kuwa ndogo lakini inatokana na uchanga wa Barnley katika ligi hiyo. Ilishiriki mwaka 2009/2010 na kushuka daraja kabla ya kupanda tena mwaka 2014/2015 ambapo Danny Ings alipanda nayo daraja akiwa na umri mdogo wa miaka 19. Ings alifunga goli lake la kwanza tar18 Aug 2014 na kwa mara ya mwisho tar.24 May 2015

 16. WATFORD - TroyDeeney - 23
Naye akiwa katika klabu changa bado kwenye Premier league, Deeney amepachika jumla ya magoli 23 tu. Maisha yake yalianzia katika klabu ya Walsall ya League One na kujiunga na Watford mwaka 2010 ambapo anaitumikia mpaka sasa. Goli lake la kwanza la ligi kuu alilifunga tar.24 Oct 2015 na mara ya mwisho kutupia ilikuwa tar. 04 Apr 2017.

17. SWANSEA CITY -  Gylfi Sigurdsson - 34
Mkali huyo wa mipira ya kutenga almaarufu "set pieces" alijiunga na Swansea akitokea Tottenham mwaka 2014 baada ya awali kuitumikia Swansea kwa mkopo. Kwa sasa anatajwa kutakiwa na klabu ya Everton huku akiwa tayari anashikilia rekodi hiyo kwa upande wa Swansea. Goli lake la kwanza alifunga tar.04 Feb 2012 na mara ya mwisho ni tar.30 Apr 2017
18. HULL CITY - Nikica Jelavic - 12
Akitoka kuitumikia Everton kwa misimu miwili, alisajiliwa na Hull mwaka 2014. Kwasasa ana umri wa miaka 31 na anaitumikia klabu ya Guizhou Hengfeng Zhicheng ya China kwa mkopo akitokea Beijing Renhe nayo ya hukohuko China. Goli lake la kwanza kwenye Premier League akiwa na Hull City ilikuwa tar. 08 Feb 2014na la mwisho tar.21 Feb 2015.


19. MIDDLESBROUGH - Hamilton Ricard - 31
Ricard ni mzaliwa wa Columbia miaka ya 1974 na aliitumikia timu ya Middlesbrough pekee Uingereza kati ya 1998- 2001akitokea Deportivo Cali, huku akicheza michezo 115. Amefunga magoli 2 tu katika mechi zisizokuwa za ligi kuu na hivyo kumfanya awe amefunga jumla ya magoli 33 akiwa Boro (Middlesbrough). Alifunga goli la kwanza tar. 29 Aug 1998 na goli la mwisho tar.21 Apr 2001






20. SUNDERLAND - Kelvin Phillips - 61
Philips ni mkongwe wa ligi ya Uingereza akitumikia timu takribani 10 za nchi hiyo. Pia yupo kwenye rekodi ya mmoja kati ya wachezaji waliofanikiwa kicheza ligi hiyo wakiwa na umri mkubwa.Pia alikuwa mfungaji bora wa premier league kwa mwaka 1999 - 2000 na amena uwezo wake kucheka na nyavu kwani akiwa na miaka 40 alifunga Hat-trick akiichezea Crystal Palace. Goli lake la kwanza kwa Sunderland ilikuwa tar.10 Aug 1999 na goli la mwisho tar.22 Feb 2003









Comments

Popular posts from this blog

ABDULRAHMAN MUSA MCHEZAJI BORA WA MWEZI LIGI KUU

Mshambuliaji Abdulrahman Musa wa JKT Ruvu ameibuka mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom kwa mwezi April 2017 Katika kinyang'anyiro hicho Mussa amewapiku Jafar Salum wa Mtibwa Sugar na Zahoro Pazi wa Mbeya City. Si mara ya kwanza kwa Abdulrahman Mussa kupeba tuzo hii ya uchezaji bora wa mwezi. Katuika msimu wa 2015/2016 Mussa alitajwa tena kuwa mchezaji bora wa ligi kuu mwezi Mey 2016 huku akiwapiku wakali kama Donald Ngoma na Ali Nassoro ambapo alicheza michezo mitatu mwezi huo na kufunga magoli 4. Mchezaji wa JKT Ruvu, Abdulrahaman Mussa (kulia) akipambana na Mshambuliaji wa  Mtibwa Sugar, Mohamed Ibrahim

Chelsea Mabingwa Wapya EPL 2016/2017

Michy Batchuayi apeleka shangwe kwa wapenzi wa "The Blue". Alazimisha sherehe ianze mapema. Sasa kurejea Stamford Bridge, Watford wakiwapoke kwa makofi kama wafalme .  Chelsea wametawazwa rasmi kuwa mabingwa wapya wa Uingereza, England Premier League baada ya kujikusanyia pointi ambazo hakuna timu yoyote kwasasa inayoweza kuzifikia. Mbelgiji Michy Batchuay ndie aliyelazimisha Chelsea kupewa tiketi ya kuanza kusherekea ubingwa wao baada ya kuipatia chelsea bao pekee dk ya 82 akiteleza kumalizia pasi iliyoingizwa na  Cesar Azpilicueta katika mchezo ulioonekana kuwa mgumu sana. Batchuayi alitokea benji akichukua nafasi ya Pedro Rodriguez katika mabadiliko mawili ya utata yaliowashangaza mashabiki wa Chelsea ambapo Eden Hazard naye alitolewa na nafasi yake kuchukuliwa na Willian. Baada ya mabadiliko haya Chelsea walianza kushambuliwa lakini ukuta wao ukiongozwa na Cahil, Luiz na Azpilicueta uliweza kuimili vishindo vya wenyeji wao. Michy Batchuayi akifunga goli 1 na l...