Skip to main content

Bayern Munich 1-2 Real Madrid: Ronaldo kanyuka 2 afunga goli la 100 UEFA

Christiano Ronaldo ameisaidia timu yake ya Real Madrid kupata ushindi wa goli 2 kwa 1 katika dimba la Alliance Arena dhidi ya wenyeji wao Bayern Munich katika mchezo wa robo fainali ya michuano ya mabingwa ulaya.
Katika ushindi huo,Ronaldo ameweka rekodi ya kufikisha idadi ya magoli 100 katika michuano hiyo ya Ulaya.
Bayern Munich ndiyo iliyoanza kupata goli kupitia kwa kiungo wao Arturo Erasmo Vidal baada ya kuunganisha krosi ya Thiago Alcantara kwa mpira wa kichwa wenye kasi mithili ya risasi na kumshinda mlinda mlango Kylo Navas.
Kunako dakika ya 45 kipindi cha kwanza, Bayern Munich walipata penati baada ya kudhaniwa kuwa Dani Carvajal aliunawa mpira eneo la 18.
Ronaldo aliipatia Real Madrid goli la kusawazisha mapema kipindi cha pili dakika ya 47 kabla ya kuhitimisha karamu ya ushindi dakika ya 77 akiunganisha mpira ulioingizwa kutoka winga ya kushoto na Marco Asensio.
Baada ya ushindi huo, Real Madrid ambao ndio mabingwa watetezi wamejiweka katika nafasi nzuri ya kutinga hatua ya nusu fainali katika mechi ya marudiano katika uwanja wao wa nyumbani wa Santiago Bernabeu mjini Madrid siku ya jumanne tarehe 18/4/2017. Hii ni kutokana na ushindi walioupata pamoja na faida ya magoli mawili ya ugenini.
Christiano Ronaldo akishangilia goli na Marco Asensio

Comments

Popular posts from this blog

Wajue Wafungaji bora wa EPL kwa kila timu inayoshiriki sasa

1. CHELSEA - Frank Lampard -147 Lampard ndiye anayeshikilia rekodi ya mfungaji bora wa Chelsea wa muda wote yaani tangu (Chelsea) ilipoanzishwa akitupia kambani magoli 211. Alisajiliwa akitokea West ham mwaka 2001 na kwa sasa ni moja kati ya mashujaa wa kubwa wa klabu ya Chelsea. Alifunga goli la kwanza la Premier League akiwa na Chelsea December 23, 2001. Goli la mwisho alilifunga 05 April 2014. 2. TOTTENHAM - Teddy Sheringham - 98 Teddy Sheringham anafahamika kama "Legend" wa Tottenham Hotspurs pamoja na kuvichezea vilabu takribani 10 vya nchini uingereza ikiwemo Manchester United na West ham United. Alisajiliwa na Tottenham akitokea Nottingham Forest mwaka 1992 na alisajiliwa na Man United 1997 kabla ya kurejea tena Tottenham 2001. Aliifungia Spurs goli la kwanza tar.02.september 1992 na la mwisho tar. 21 April 2003 kabla hajatimkia Portsmouth   3. MANCHESTER CITY - Sergio Aguero -120 Akiwa amesaliwa na magoli 10 tu kuwa mfungaji bora wa historia wa M...

ABDULRAHMAN MUSA MCHEZAJI BORA WA MWEZI LIGI KUU

Mshambuliaji Abdulrahman Musa wa JKT Ruvu ameibuka mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom kwa mwezi April 2017 Katika kinyang'anyiro hicho Mussa amewapiku Jafar Salum wa Mtibwa Sugar na Zahoro Pazi wa Mbeya City. Si mara ya kwanza kwa Abdulrahman Mussa kupeba tuzo hii ya uchezaji bora wa mwezi. Katuika msimu wa 2015/2016 Mussa alitajwa tena kuwa mchezaji bora wa ligi kuu mwezi Mey 2016 huku akiwapiku wakali kama Donald Ngoma na Ali Nassoro ambapo alicheza michezo mitatu mwezi huo na kufunga magoli 4. Mchezaji wa JKT Ruvu, Abdulrahaman Mussa (kulia) akipambana na Mshambuliaji wa  Mtibwa Sugar, Mohamed Ibrahim

Chelsea Mabingwa Wapya EPL 2016/2017

Michy Batchuayi apeleka shangwe kwa wapenzi wa "The Blue". Alazimisha sherehe ianze mapema. Sasa kurejea Stamford Bridge, Watford wakiwapoke kwa makofi kama wafalme .  Chelsea wametawazwa rasmi kuwa mabingwa wapya wa Uingereza, England Premier League baada ya kujikusanyia pointi ambazo hakuna timu yoyote kwasasa inayoweza kuzifikia. Mbelgiji Michy Batchuay ndie aliyelazimisha Chelsea kupewa tiketi ya kuanza kusherekea ubingwa wao baada ya kuipatia chelsea bao pekee dk ya 82 akiteleza kumalizia pasi iliyoingizwa na  Cesar Azpilicueta katika mchezo ulioonekana kuwa mgumu sana. Batchuayi alitokea benji akichukua nafasi ya Pedro Rodriguez katika mabadiliko mawili ya utata yaliowashangaza mashabiki wa Chelsea ambapo Eden Hazard naye alitolewa na nafasi yake kuchukuliwa na Willian. Baada ya mabadiliko haya Chelsea walianza kushambuliwa lakini ukuta wao ukiongozwa na Cahil, Luiz na Azpilicueta uliweza kuimili vishindo vya wenyeji wao. Michy Batchuayi akifunga goli 1 na l...