Ripoti zinasema kuwa kiungo wa Chelsea Eden Hazard
amezungumza na rafiki zake na kuwaambia kuwa anataka kujiunga na real
Madeid ili kushinda tuzo ya mchezaji
bora wa dunia.
Kiungo huyo wa ubelgiji amekuwa katika rada ya Real Madrid
baada ya kuwa katika kiwango kizuri kwa misimu kadhaa sasa akiwa na ‘the
Blues’.
Mara kadhaa Hazard amekuwa akitoa kauli zisizoonyesha hasa
uelekeo wake ni upi baada ya kumalizika kwa msimu huu, japokuwa kwa mujibu wa
mkataba wake mpaka sasa, Hazard ana muda wa miaka 3 ya kuitumikia Chelsea.
Alipowahi kuuulizwa kuhusu hatima yake, Hazard amesema
“Suala hilo halipo
kwenye akili yangu kwa sasa. Nachojua ni kwamba nina miaka 2 au 3 iliyobaki
katika mkataba wangu. Nahitaji kumaliza msimu na kisha tutajua nini
kinaendelea".
Katika hatua nyingine taarifa zinasema kuwa uongozi wa klabu
ya Chelsea upo katika harakati za kumuita mezani Hazard kwa mazungumzo ya
kumpati a mkataba mwingine.
Comments
Post a Comment