Skip to main content

Liverpool kuwakumbuka 96 waliokufa janga la Hillsborough: Ifahamu zaidi "HILLSBOROUGH DISASTER"

Familia ya wana Liverpool FC wakiwemo wakiwemo mashabiki, wachezaji, Viongozi wa timu pamoja na wanafamilia na wahanga wa janga la Hillsborough (Hillsborough Family Support Group -HFSG) wataungana leo katika maadhimisho ya kuwakumbuka wapendwa wao waliofariki tarehe kama ya leo miaka 28 iliyopita wakiwa uwanjani.

Tukio hilo maarufu kama "HILLSBOROUGH DISASTER 96" lilitokea katika mchezo wa nusu fainali ya mwaka 1988-1989 kati ya Liverpool na Nottingham Forest katika uwanja wa Hillsborough .Katika tukio hili watu 96 walifariki dunia na wengine 766 kujeruhiwa na kuacha kumbukumbu mpaka leo yakuwa ni janga kubwa la kimichezo kuwahi kutokea katika hisporia ya michezo Uingereza.

Chanzo cha tukio hili ni amri ya kimakosa ya Afisa polisi ambaye ni mkuu wa siku hiyo Police David Duckenfield iliyoamuru geti la kuingia uwanjani lililojulikana kama Geti "C" kufunguliwa angali nje kulikuwa na idadi kubwa ya mashabiki waliokuwa wakishinikiza kuingia ndani.
Baada ya geti hilo kufunguliwa, mashabiki waliingia kwa fujo uwanjani na kupelekea jukwaa moja kuzidiwa, jukwaa ambalo hatahivyo lilisemekana kuwa tayari lilikuwa  na watu wengi kabla. Hali hii ilipelekea nguzo za juu za uwanja huo kuanguka na kusababisha vifo na majeruhi hao.



Jeshi la police la uingereza lilitoa taarifa iliyoonekana kuwa ni ya uongo kwa kusema kuwa ni Ulevi wa mashabiki wa Liverpool uliopelekea kutokea kwa maafa hayo.
Awamu mbalimbali za watafiti zilifanyika ili kubainisha chanzo hasa cha maafa hayo na utafiti wa mwisho ulifanyika April 2014 hadi April 2016 na kutoa hitimisho kuwa yalikuwa ni makosa ya mamlaka ya polisi pamoja na watu wa huduma ya ambulance kwa kushindwa kudhibiti usalama na kupelekea vifo kwa wasio na hatia.
Tofauti na miaka mingine ilivyozoeleka, maadhimisho ya mwaka huu hayatofanyika katika uwanja wa Anfield na badala yake yatafanyika kanisa la kianglikan la mjini Liverpool kufuatia maombi ya muunganiko wa wanafamilia na wahanga wa Hillsborough yaani Hillsborough Family Support Group yaliyoafikiwa mwaka jana na kutaka maadhimisho ya 2016 yawe ya mwisho kufanyika uwanjani hapo.

Wachezaji na wafanyakazi wa Liverpool wataonyesha heshima yao kwa kumbukumbu ya tukio hilo leo katika mazoezi pale ambao filimbi itapulizwa wakiwa katikati ya mazoezi wakati timu hiyo ikijiandaa kuwakabili West Bromwich Albion na kutulia kimya kwa dakika kadhaa ifikapo saa 3:06PM muda ambao ndipo refa wa mechi ya FA 1989 alipuliza kipenda kusimamisha mpira kufuatia tukio hilo.
Katika tukio hilo kocha Jurgen Klopp na nahodha Jordan Henderson wataweka maua sehemu iliyoandaliwa kama kumbukumbu na heshima kwa mashabiki wa liverpool waliofariki kipindi hicho.

Klopp amesema siku hiyo ni ya muhimu kwa wanafamilia wote wa mpira wa miguu na zaidi kwao na kuongeza kuwa wanajua ni tukio la muhimu kwa wanafamilia wa wahanga hao na suala la kutoadhimisha tukio hilo Anfield haliwafanyi waache kuwakumbuka wapenzi wao.









Comments

Popular posts from this blog

Wajue Wafungaji bora wa EPL kwa kila timu inayoshiriki sasa

1. CHELSEA - Frank Lampard -147 Lampard ndiye anayeshikilia rekodi ya mfungaji bora wa Chelsea wa muda wote yaani tangu (Chelsea) ilipoanzishwa akitupia kambani magoli 211. Alisajiliwa akitokea West ham mwaka 2001 na kwa sasa ni moja kati ya mashujaa wa kubwa wa klabu ya Chelsea. Alifunga goli la kwanza la Premier League akiwa na Chelsea December 23, 2001. Goli la mwisho alilifunga 05 April 2014. 2. TOTTENHAM - Teddy Sheringham - 98 Teddy Sheringham anafahamika kama "Legend" wa Tottenham Hotspurs pamoja na kuvichezea vilabu takribani 10 vya nchini uingereza ikiwemo Manchester United na West ham United. Alisajiliwa na Tottenham akitokea Nottingham Forest mwaka 1992 na alisajiliwa na Man United 1997 kabla ya kurejea tena Tottenham 2001. Aliifungia Spurs goli la kwanza tar.02.september 1992 na la mwisho tar. 21 April 2003 kabla hajatimkia Portsmouth   3. MANCHESTER CITY - Sergio Aguero -120 Akiwa amesaliwa na magoli 10 tu kuwa mfungaji bora wa historia wa M...

ABDULRAHMAN MUSA MCHEZAJI BORA WA MWEZI LIGI KUU

Mshambuliaji Abdulrahman Musa wa JKT Ruvu ameibuka mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom kwa mwezi April 2017 Katika kinyang'anyiro hicho Mussa amewapiku Jafar Salum wa Mtibwa Sugar na Zahoro Pazi wa Mbeya City. Si mara ya kwanza kwa Abdulrahman Mussa kupeba tuzo hii ya uchezaji bora wa mwezi. Katuika msimu wa 2015/2016 Mussa alitajwa tena kuwa mchezaji bora wa ligi kuu mwezi Mey 2016 huku akiwapiku wakali kama Donald Ngoma na Ali Nassoro ambapo alicheza michezo mitatu mwezi huo na kufunga magoli 4. Mchezaji wa JKT Ruvu, Abdulrahaman Mussa (kulia) akipambana na Mshambuliaji wa  Mtibwa Sugar, Mohamed Ibrahim

Chelsea Mabingwa Wapya EPL 2016/2017

Michy Batchuayi apeleka shangwe kwa wapenzi wa "The Blue". Alazimisha sherehe ianze mapema. Sasa kurejea Stamford Bridge, Watford wakiwapoke kwa makofi kama wafalme .  Chelsea wametawazwa rasmi kuwa mabingwa wapya wa Uingereza, England Premier League baada ya kujikusanyia pointi ambazo hakuna timu yoyote kwasasa inayoweza kuzifikia. Mbelgiji Michy Batchuay ndie aliyelazimisha Chelsea kupewa tiketi ya kuanza kusherekea ubingwa wao baada ya kuipatia chelsea bao pekee dk ya 82 akiteleza kumalizia pasi iliyoingizwa na  Cesar Azpilicueta katika mchezo ulioonekana kuwa mgumu sana. Batchuayi alitokea benji akichukua nafasi ya Pedro Rodriguez katika mabadiliko mawili ya utata yaliowashangaza mashabiki wa Chelsea ambapo Eden Hazard naye alitolewa na nafasi yake kuchukuliwa na Willian. Baada ya mabadiliko haya Chelsea walianza kushambuliwa lakini ukuta wao ukiongozwa na Cahil, Luiz na Azpilicueta uliweza kuimili vishindo vya wenyeji wao. Michy Batchuayi akifunga goli 1 na l...