Mshambuliaji kinda wa AS Monaco ya Ufaransa Kylian Mbappe mwenye umri wa miaka 18 ametangazwa kuwa mchezaji bora wa wiki wa michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya.
Mbappe aliyekuwa na mchango mkubwa katika kuivusha timu yake kwenda hatua ya nusu fainali, amepata tuzo hiyo ya UEFA POTW (UEFA Player Of The Week) kwa kuwabwaga nyota kama Cristiano Ronaldo, Paulo Dybala na Antoine Griezmann baada ya kuwazidi kwa kura.
Katika ushindi wa jumla yaani Aggregates Monaco ilishinda kwa magoli 6-3 dhidi ya Borrusia Dortmund ambapo katika mchezo wa kwanza Mbappe aliipatia timu yake ya Monaco magoli 2 kabla ya kukamilisha karamu hiyo kwa goli 1 katika mchezo wa marudiano mjini Monaco, Ufaransa.

Comments
Post a Comment