Winga wa Liverpool Sadio Mane anahatihati ya kuukosa mchezo wa ligi kuu dhidi ya Bournemouth utakaopigwa katika dimba la Anfield siku ya jumatano kufuatia kuumia katika mechi dhidi ya Everton.
Mane aliumia alipokuwa akiwania mpira dhidi ya beki wa kushoto wa Everton Leighton Baines katika ushindi wa 3-1 ambao liverpool iliupata.
Mane kuukosa mchezo dhidi ya Bournemouth unaoonekana kuja mapema sana kwake, ni pengo kwa Liverpool hasa ikizingatiwa kuwa Liverpool ilipoteza mchezo wa kwanza dhidi yao kwa goli 3-4.
Kama haitoshi, ni mabadiliko yaliyofanywa kwa kumtoa Mane katika mchezo huo ndipo magoli yote yalirudishwa ambapo awali Liverpool ilikuwa ikiongoza kwa magoli 3-1.
Mane atasubiri kufanyiwa vipimo vya "scan" ilikutathmini ameumia kwa kiasi gani kabla ya kubainika atatakiwa kupata matibabu kwa muda gani. Hata hivyo mshambuliaji huyo aliwashangaza waandishi alipokutana nao baada ya mchezo kumalizika kwa kuwaambia hana shida yoyote.
Walter. S
Mane aliumia alipokuwa akiwania mpira dhidi ya beki wa kushoto wa Everton Leighton Baines katika ushindi wa 3-1 ambao liverpool iliupata.
Mane kuukosa mchezo dhidi ya Bournemouth unaoonekana kuja mapema sana kwake, ni pengo kwa Liverpool hasa ikizingatiwa kuwa Liverpool ilipoteza mchezo wa kwanza dhidi yao kwa goli 3-4.
Kama haitoshi, ni mabadiliko yaliyofanywa kwa kumtoa Mane katika mchezo huo ndipo magoli yote yalirudishwa ambapo awali Liverpool ilikuwa ikiongoza kwa magoli 3-1.
Walter. S
Comments
Post a Comment