Brighton & Hove Albion imefanikiwa kupanda daraja na hivyo kushiriki ligi kuu ya uingereza msimu ujao baada ya kujikusanyia jumla ya point 79 katika michezo 43 iliyokwisha cheza mpaka sasa ikiwa imesalia michezo 3.
Brighton Albion inayonolewa na kocha wa zamani wa Birmingham City na Norwich City, Chris Hughton itakuwa ni timu ya 48 kushiriki ligi kuu ya uingereza baada ya kupata ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya Wigan Athletics siku ya jumatatu.
Kwa upande wake kocha Hughton amesema kuwa anajivunia namna ambavyo timu hiyo walivyojirudi kwa kasi kufuatia hali ya msimu. Aidha ameongeza kuwa kuweka nguvu zao kwa pamoja hadi kufikia hatua hii sio jambo rahisi, na wanahitaji kila aina ya pongezi.
Brighton walinusa nafasi ya kucheza ligi kuu ya uingereza msimu uliopita baada ya kuwa katika ushindani mkubwa na kujikuta wakipoteza nafasi hiyo kwa tofauti ya magoli ya kufungwa na kufunga dhidi ya Barnely kufuatia matokeo ya sare waliyoyapata dhidi Middlesbrough.
Kufuatia ushindi huu wa "the Albion" mashabiki wa timu hiyo walikusanyika katikati ya uwanja kusherekea timu yao kupanda daraja.
Brighton inatumia uwanja unaoitwa "FALMER STADIUM" unaodhaminiwa na American Express na kuufanya ujulikane kama "Amex Stadium" wenye uwezo wa kubeba idadi ya mashabiki 30,750
Mbali na mafanikio haya, Brighton Albion wamewahi kufikia mafanikio mengine ikiwemo kushiriki na kufika fainali katika michuano ya FA mwaka 1983 dhidi ya Manchester United ambapo Manchester United walishinda kwa magoli 4-0 baada ya mchezo wa kwanza kutoshana kwa 0-0.
Hao ndio Brighton & Hove Albion waliojikatia ticket ya kushiriki ligi kuu msimu ujao watakapokutana na wapinzani wao wa jadi ambao ni Crystal Palace
Brighton Albion inayonolewa na kocha wa zamani wa Birmingham City na Norwich City, Chris Hughton itakuwa ni timu ya 48 kushiriki ligi kuu ya uingereza baada ya kupata ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya Wigan Athletics siku ya jumatatu.
Kwa upande wake kocha Hughton amesema kuwa anajivunia namna ambavyo timu hiyo walivyojirudi kwa kasi kufuatia hali ya msimu. Aidha ameongeza kuwa kuweka nguvu zao kwa pamoja hadi kufikia hatua hii sio jambo rahisi, na wanahitaji kila aina ya pongezi.
Brighton walinusa nafasi ya kucheza ligi kuu ya uingereza msimu uliopita baada ya kuwa katika ushindani mkubwa na kujikuta wakipoteza nafasi hiyo kwa tofauti ya magoli ya kufungwa na kufunga dhidi ya Barnely kufuatia matokeo ya sare waliyoyapata dhidi Middlesbrough.
Kufuatia ushindi huu wa "the Albion" mashabiki wa timu hiyo walikusanyika katikati ya uwanja kusherekea timu yao kupanda daraja.
Mashabiki wa Brighton wakiwa uwanjani baada ya mechi dhidi ya Wigan wakisherekea kupanda daraja kwa timu hiyo |
Mbali na mafanikio haya, Brighton Albion wamewahi kufikia mafanikio mengine ikiwemo kushiriki na kufika fainali katika michuano ya FA mwaka 1983 dhidi ya Manchester United ambapo Manchester United walishinda kwa magoli 4-0 baada ya mchezo wa kwanza kutoshana kwa 0-0.
Hao ndio Brighton & Hove Albion waliojikatia ticket ya kushiriki ligi kuu msimu ujao watakapokutana na wapinzani wao wa jadi ambao ni Crystal Palace
Mchezaji wa Brighton Glenn Murray aliyefunga goli la kwanza akishangilia huku akipiga Selfie |
Comments
Post a Comment