UEFA
Droo ya ligi ya mabingwa barani ulaya imefanyika hii leo huku mabingwa watetezi Real Madrid wakipangwa kukutana na wapinzani wao wa jadi Athletico Madric na Juventus wakipangwa na AS Monaco.Real Madrid watakuwa wanakutana na Athletico Madrid mara ya 3 katika miaka 4 iliyopita ambapo wamekutana katika fainali mwaka 2014 na 2016 huku Real Madrid akifanikiwa kumtambia mwenzake kwa mara zote mbili.
Mwaka huu Real Madrid atakutana na Athletico katika hatua ya nusu fainali huku vijana hao wa Zinadine wakinuwia kuweka historia ya kulichukua kombe hilo mara 2 mfululizo, historia ambayo haijawahi kutokea katika michuano hii.
Real Madrid ndio watakaoanza kwa kuwakaribisha wapinzania wao katika dimba la Santiago Bernabeu tarehe 2 May kabla ya kurudiana katika uwanja wa Vicente Calderon May,10.
Kwingineko, Vibibi vizee vya Turin huko Italy, Juventus wao watamenyana na AS Monaco tarehe 3 May na watarudiana tarehe 9 may. Timu hizo zimekutana katika michuano hii kwa mara ya mwisho mwaka 1997/98.
Comments
Post a Comment