- Calum Chambers apewa kazi ya kufanya.
- Lukaku naye ana adhma ya kurejea kwenye mbio za "Golden boot"
Mlinzi wa Arsenal Calum Chambers akimdhibiti Sadio Mane katika mechi ya kwanza ya ligi |
Kocha Steve Agnew amesema kuwa Arsenal imeweka matumaini makubwa kwa mchezaji wao anayeitumikia Middlesbrough kwa mkopo Calum Chambers na wamekuwa wakimtumia jumbe za kumpa ujasiri katika mchezo huo utakaopigwa Anfield.
Arsenal ipo nyuma ya Liverpool kwa alama moja wakijikusanyia alama 73 na liverpool wakiwa na alama 72 huku wote wakisaliwa na mchezo mmoja wa kumalizia ligi hapo kesho. Michezo yote miwili (pamoja mingine yote ya ligi) itapigwa muda mmoja wakati Liverpool watawakaribisha Middlesbrough na Arsenal watawakaribisha Everton.
Katika hatua nyingine, Arsenal atakuwa na kibarua kizito katika mechi yake dhidi ya Everton na ugumu wa mechi hiyo utachagizwa na Lukaku ambaye atakuwa anahitaji magoli mawili au zaidi ili kubakisha matumaini yake ya kukiwania kiatu cha dhahabu.
Kwasasa Lukaku ana magoli 24 huku Harry Kane akiwa ana magoli 26 baada ya kuonekana mwiba mchingu katika mechi dhidi ya Leicester City alhamis ya juzi, ambapo alifunga magoli manne katika ushindi wa magoli 6-1.
Wakati Everton wakijitahidi kumtengenezea Lukaku nafasi za magoli, Watakuwa pia wakimzuia Sanchez asiongeze magoli kwani naye yupo nyuma ya Lukaku kwa tofauti ya goli 1.
Hali hii inafanya mchezo kati ya Arsenal na Everton pamoja na wa Liverpool na Middlesbrough kuwa na msisimko wa aina yake.
Comments
Post a Comment