Nchini Uingereza kulikuwa na mchezo wa kiporo baina ya Arsenal waliokuwa ugenini kuikabili Southampton ikisaka point 3 muhimu za kurejesha matumaini ya kusalia nafasi ya nne bora. Katika mchezo huo Arsenal imefanikiwa
kipata ushindi wa goli 2 bila dhidi ya Southampton ambao waliokuwa
katika uwanja wao wa nyumbani wa St. Marys.
Goli la kwanza la Arsenal lilipachikwa wavuni na mshambuliaji wao Alexis Sanches dakika ya 60 akipokea pasi kutoka kwa Mesut Ozil na kuwahadaa walinzi wa St. Marys.
Goli la pili lilifungwa na Olivier Giroud dakika ya 83 aliyetokea benji kuchukua nafasi ya Danny Welbeck baada ya kupasiana pasi za vichwa na Aaron Ramsey naye kumalizia kwa kichwa na mpira kumshinda mlinda mlango Fraser Foster
.
Ushindi huo unawaweka Arsenal katika nafasi ya 5 huku Manchester United ikishuka hadi nafasi ya 6 kwenye msimamo wa ligi kuu Uingereza.
Goli la kwanza la Arsenal lilipachikwa wavuni na mshambuliaji wao Alexis Sanches dakika ya 60 akipokea pasi kutoka kwa Mesut Ozil na kuwahadaa walinzi wa St. Marys.
Sanches akishangilia baada ya kufunga goli la 1 |
Olivier Giroud akifunga goli la pili |
.
Ushindi huo unawaweka Arsenal katika nafasi ya 5 huku Manchester United ikishuka hadi nafasi ya 6 kwenye msimamo wa ligi kuu Uingereza.
Comments
Post a Comment