Skip to main content

Kipa wa Chelsea Asmir Begovic atimkia FC Bournemouth

Klabu ya FC Bournemouth imemsajili kipa Asmir Begovic kutoka Chelsea kwa ada ambayo bado halijawekwa wazi mpaka sasa.
Chelsea ilimsajili Begovic kutoka Stoke City alikoitumikia kwa mafanikio kwa kucheza jumla ya mechi 160 huku pamoja na kucheza nafasi hiyo, alibahatika kuifungia Stoke goli moja ambalo ndio pekee katika michezo 259 aliyoshuka uwanjani na vilabu mbali mbali.
Begovic (29) anaenda kuitumikia Bournemouth kwa mara ya pili akiwa ameshawahi kuichezea kwa mkopo akitokea klabu ya Portsmouth mwaka 2007.

Pamoja na dau hilo kutowekwa wazi, inasemekana kuwa Begovic ameuzwa kwa ada ya paundi mil.10 huku tayari Chelsea ikiwa imeanza mbio za kumuwania mlinzi wa PSG Alphonse Areola (24) ili kuziba pengo la Begovic.
Begovic ameichezea chelsea jumla ya mechi 19, tangu aliposajiliwa akitokea Stoke, huku akishindwa kujiimarisha kama kipa namba moja wa chelsea kutokana na chaguo la kwanza kuwa ni mbelgiji Thibaut Courtois.
Baada ya kukamilisha usajili huo, mlinzi huyo kutoka Bosnia na Herzegovina alikuwa na haya ya kusema kupitia ukurasa wake wa twitter.
"Asante wachezaji wenzangu, kocha, wafanyakazi na mashabiki wa Chelsea. Ilikuwa ni faraja kuwa sehemu ya kikosi hiki cha ushindi. Nawatakia mazuri huko mbeleni"
Alisema Begovic kupitia ukurasa wake wa twitter ambapo aliambatanisha na picha za kushangilia ushindi akiwa wachezaji wa chelsea. Pia alituma ujumbe mwingine akisema kuwa anayofuraha kujiunga na FC Bournemouth na anatazamia kujituma kuisaidia timu hiyo.
Begovic anakuwa ni mchezaji wa kwanza kuondoka katika kikosi hicho cha mabingwa wa Uingereza msimu 2016/2017.
Kipa wa zamani wa Chelsea Asmir Begovic akisaini mkataba na klabu ya FC Bournemouth

Begovic akiwa 'amepoz' na skafu ya klabu yake mpya ya Bournemouth baada ya kusaini mkataba

Comments

Popular posts from this blog

Wajue Wafungaji bora wa EPL kwa kila timu inayoshiriki sasa

1. CHELSEA - Frank Lampard -147 Lampard ndiye anayeshikilia rekodi ya mfungaji bora wa Chelsea wa muda wote yaani tangu (Chelsea) ilipoanzishwa akitupia kambani magoli 211. Alisajiliwa akitokea West ham mwaka 2001 na kwa sasa ni moja kati ya mashujaa wa kubwa wa klabu ya Chelsea. Alifunga goli la kwanza la Premier League akiwa na Chelsea December 23, 2001. Goli la mwisho alilifunga 05 April 2014. 2. TOTTENHAM - Teddy Sheringham - 98 Teddy Sheringham anafahamika kama "Legend" wa Tottenham Hotspurs pamoja na kuvichezea vilabu takribani 10 vya nchini uingereza ikiwemo Manchester United na West ham United. Alisajiliwa na Tottenham akitokea Nottingham Forest mwaka 1992 na alisajiliwa na Man United 1997 kabla ya kurejea tena Tottenham 2001. Aliifungia Spurs goli la kwanza tar.02.september 1992 na la mwisho tar. 21 April 2003 kabla hajatimkia Portsmouth   3. MANCHESTER CITY - Sergio Aguero -120 Akiwa amesaliwa na magoli 10 tu kuwa mfungaji bora wa historia wa M...

ABDULRAHMAN MUSA MCHEZAJI BORA WA MWEZI LIGI KUU

Mshambuliaji Abdulrahman Musa wa JKT Ruvu ameibuka mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom kwa mwezi April 2017 Katika kinyang'anyiro hicho Mussa amewapiku Jafar Salum wa Mtibwa Sugar na Zahoro Pazi wa Mbeya City. Si mara ya kwanza kwa Abdulrahman Mussa kupeba tuzo hii ya uchezaji bora wa mwezi. Katuika msimu wa 2015/2016 Mussa alitajwa tena kuwa mchezaji bora wa ligi kuu mwezi Mey 2016 huku akiwapiku wakali kama Donald Ngoma na Ali Nassoro ambapo alicheza michezo mitatu mwezi huo na kufunga magoli 4. Mchezaji wa JKT Ruvu, Abdulrahaman Mussa (kulia) akipambana na Mshambuliaji wa  Mtibwa Sugar, Mohamed Ibrahim

Chelsea Mabingwa Wapya EPL 2016/2017

Michy Batchuayi apeleka shangwe kwa wapenzi wa "The Blue". Alazimisha sherehe ianze mapema. Sasa kurejea Stamford Bridge, Watford wakiwapoke kwa makofi kama wafalme .  Chelsea wametawazwa rasmi kuwa mabingwa wapya wa Uingereza, England Premier League baada ya kujikusanyia pointi ambazo hakuna timu yoyote kwasasa inayoweza kuzifikia. Mbelgiji Michy Batchuay ndie aliyelazimisha Chelsea kupewa tiketi ya kuanza kusherekea ubingwa wao baada ya kuipatia chelsea bao pekee dk ya 82 akiteleza kumalizia pasi iliyoingizwa na  Cesar Azpilicueta katika mchezo ulioonekana kuwa mgumu sana. Batchuayi alitokea benji akichukua nafasi ya Pedro Rodriguez katika mabadiliko mawili ya utata yaliowashangaza mashabiki wa Chelsea ambapo Eden Hazard naye alitolewa na nafasi yake kuchukuliwa na Willian. Baada ya mabadiliko haya Chelsea walianza kushambuliwa lakini ukuta wao ukiongozwa na Cahil, Luiz na Azpilicueta uliweza kuimili vishindo vya wenyeji wao. Michy Batchuayi akifunga goli 1 na l...