Manchester City wanakaribia kuinasa saini ya mlinzi wa Benifica, Mbrazili Ederson Moraes kufuatia mazungumzo na klabu hiyo wiki iliyopita.
Manchester City wameweka mezani ofa ya paundi milioni 43 kiasi kinachotajwa kuvunja rekodi ya usajili kwa nafasi hiyo ya uchezaji. Mlinzi wa Juventus Gianluigi Buffon ndiye anayeshikilia rekodi hiyo baada ya kusajiliwa kwa paundi mil 32 akitokea Parma mwaka 2001.
Kwingineko kupitia jarida la The Sun, habari zinasema kuwa kipa huyo anatarajia kupanda ndege leo kuja jijini Manchester kukamilisha usajili huo.
Usajili wa Ederson unakuja ikiwa ni siku chache tu baada ya Man City kufungua milango kwa kipa wao Willy Caballero kuondoka klabuni hapo. Hata hivyo uwepo wa kipa namba moja kwasasa Claudio Bravo aliyesajiliwa mwaka jana akitokea Barcelona haumfanyi kocha Pep Guardiola kujiamini kutokana na makosa ambayo ameukuwa akiyafanya langoni.
Machester City pia ina hazina ya mlinda mlango wa muda mrefu Joe Hart ambaye anatarajiwa kurejea kutoka Torino alipokuwa kwa mkopo. Hata hivyo Joe Hart anaonekana kutokuwa chaguo sahihi la kocha Guardiola.
Endapo Ederson atasajiliwa na Man City, utakuwa ni usajili wa pili kukamilika kufuatia City kukamilisha usajili wa kiungo Bernando Silva kutoka Monaco mwishoni mwa wiki iliyopita.

Comments
Post a Comment