Klabu ya Barcelona imemthibitisha Ernesto Valverde (53) kuwa kocha mpya wa timu hiyo baada ya Kocha huyo kuafiki makubaliano na vigogo hao wa Catalunia.
Valverde aliyekuwa kocha wa Althetico Bilbao atasaini mkataba wa awali wa kuinoa Barcelona kwa miaka miwili.
Kama ilivyo desturi ya Barcelona kupendelea kuwapa ukocha wachezaji wa zamani wa klabu hiyo, Valverde naye alishaitumikia Barcelona kati ya mwaka 1988 hadi 1990.
Valverde amekuwa na uzoefu mkubwa katika ukocha akizifundisha timu takribani 6 huku akiifundisha Athletico Bilbao mara tatu katikavipindi tofauti, mara akiwa kama kocha msaidizi na mara mbili akiwa kama kocha mkuu.
Pia alishaifundisha Olimpiacos ya ugiriki kwa awamu mbili tofauti. Mara ya kwanza 2008/2009 akitokea Espanyol na mara ya pili 2010-2012 akitokea Villareal aliyoifundisha kwa mwaka mmoja. Baada ya hapo aliifundisha Valencia 2012-2013 na baadae Athletico Bilbao 2013-2017
VILABU ALIVYOFUNDISHA VALVERDE
KIPINDI TIMU
2001–2002 ATHLETICO BILBAO (Kocha Msaidizi)
2002–2003 BILBAO ATHLETIC
2003–2005 ATHLETICO BILBAO
2006–2008 ESPANYOL
2008–2009 OLIMPIACOS
2009–2010 VILLAREAL
2010–2012 OLIMPIACOS
2012–2013 VALENCIA
2013–2017 ATHLETICO BILBAO
2017– BARCELONA - (SASA)
Kabla ya kuwa kocha, Valverde aliwahi kucheza mpira kama mshambuliaji katika vilabu mbalimbali ikiwemo Alaves,Sestao, Espanyol, Barcelona, Athletico Bilbao na Real Mallorca zote za nchini Hispania.
Comments
Post a Comment