Harry Kane jana amejitakatisha kileleni mwa orodha ya wafungaji bora wa EPL baada ya kufunga magoli 4 katika ushindi wa magoli 6 kwa 1 dhidi ya Leicester City.
Kufuatia ushindi huo, Kane sasa anaongoza mbio za kukipata kiatu cha dhahabu kwa kumzidi Lukaku kwa magoli mawili, yeye akiwa na magoli 26 na Lukaku 24.
Kane alifunga goli la kwanza dakika ya 25 akipokea pasi kutoka kwa Heung-Min Son. Baada ya dakika 11 Heung-Min Son aliipatia Spurs goli la pili akipokea pasi kutoka kwa muingereza Dele Ali.
Leicester City walipata goli la kufutia machozi kipindi cha pili dk ya 59 kupitia kwa mlizi wao Ben Chilwell lakini hata hivyo lilishindwa kuwaongezea munkari wa kubadili matokeo.
Harry Kane alirudi tena kambani kunako dk ya 63 akimalizia jitihada zilizofanywa na Victor Wanyama baada ya mpira wa kichwa uliopigwa kuokolewa na mchezaji wa Leicester.
Kunako dakika ya 71 Heung-Min Son kwa mara nyingine aliiandikia Spurs goli la 4, muda huu Kane akirudisha fadhila kwa Son kwa kutoa pasi ya mwisho.
Tottenham waliendelea kulisakama lango la Leicester kama simba mwenye njaa na zikiwa zimesalia dakika 2 kabla ya kukamilika dakika 90 Harry Kane alitupia goli la 3 na kukamilisha Hat-trick dk 88 akipokea pasi toka kwa Filip Lesniak. Njaa ya kukinyakua kiatu cha dhahabu haikuishia hapo kwa Harry Kane kwani baada muda wa nyongeza kujulikana Kane alikwamisha wavuni goli la nne akipokea pasi kutoka kwa Ben Davies

Comments
Post a Comment