Mchezaji bora wa mwaka jana wa ligi kuu ya Uingereza Riyad Mahrez amesema anataka kuondoka Leicester City msimu huu wa majira ya joto.
Mahrez amesema kuwa amekuwa na shauku ya kuendeleza soka lake sehemu nyingine na walikubaliana na klabu kuwa angesalia hapo King Power kwa mwaka mmoja tu hivyo muda umekwisha.
Mualgeria huyo mwenye umri wa miaka 26 aliisaidia Leicester City kunyakua ubingwa wa Premier League msimu uliopita wa mwaka 2015/2016.
Mahrez pia ameisaidia timu hiyo kusalia katika ligi kuu msimu huu kwa kupachika wavuni magoli 10, baada ya kusuasua katika michezo ya mzunguko wa kwanza wa ligi lakini kama haitoshi pia ameisaidia kufika hadi hatua ya robo fainali katika michuano ya ligi kuu ya mabingwa ulaya.
"Pamoja na kuwa naihusudu na kuiheshimu Leicester City, napenda kuwa mkweli na muwazi. Nimeongea na klabu yangu na nimewaambia kuwa nadhani sasa ni muda muafaka wa kuendelea mbele" Mahrez alisema.
"Nimekuwa na maongezi mazuri tu na mwenyekiti msimu uliopita na tulikubaliana kwa muda ule kuwa nitakaa kwa mwaka mmoja mwingine ili niisaidie timu yangu kwa nguvu zote kufuatia kipindi cha mpito toka kubeba ubingwa na kucheza Champions League".
"Nimekuwa na misimu minne mizuri na Leicester na nimefurahia kila wakati nilipokuwa hapa. Najihisi mwenye ufahari mkubwa kuwa sehemu ya mafanikio tuliyoyapata nikiwa hapa, ikiwemo kuwa mabingwa wa ligi kuu.
"Mahusiano niliyoshea na klabu na mashabiki hawa wazuri, ni moja ya vitu nitakavyovikumbuka milele na naamini wataelewa na kuheshimu maamuzi yangu". Alimalizia Mahrez ambaye alisajiliwa na Leicester mwaka 2014 akitokea Le Harve ya Ufaransa.
TUFUATILIE KUPITIA FACEBOOK NA TWITTER
Bofya hapa chini ku-like ukurasa wetu wa facebook
https://www.facebook.com/RadaYetuSports/
Bofya hapa kutufuatilia kupitia twitter
https://twitter.com/RadaYetu

Comments
Post a Comment