Manchester united chini ya kocha Jose Mourinho imetwaa Kombe la Uefa Europa league baada ya kuilaza Ajax kwa magoli 2-0.
Kwa ushindi huo Manchester inakata tiketi ya kushiriki michuano ya ligi ya mabingwa ulaya na moja kwa moja wataingia kwenye hatua ya makundi.
Goli la kwanza la Manchester lilifungwa na Paul Pogba dakika ya baada ya kuwekewa mpira na fellaini na kuutenga kabla ya kupiga shuti lililomgusa mlinzi wa Ajax Davinson Sanchez na kumpoteza kipa Andre Onana.
Goli la pili lilifungwa kipindi cha pili kupitia kwa Henrik Mkhitaryan baada ya kuunganisha mpira uliokuwa ukitaka kuokolewa kwa kichwa na mchezaji wa Ajax.
Hata hivyo Ajax ndio waliowaandama Manchester united licha ya kuonekana wazi kuwa mbinu za kupenya ukuta wa Mashetani hao kugonga mwamba.
Kombe hili linaifanya Manchester united kuwa klabu ya kwanza ya uingereza kuwazidi Liverpool kwa vikombe kwani kwasasa watakuwa na vikombe 42 dhidi ya Liverpool yenye jumla ya vikombe 41.
Comments
Post a Comment