Kiungo mwenye kipaji kutoka Ubelgiji Youri Tielemans amesajiliwa na klabu ya AS Monaco kwa ada inayokadiriwa kufikia paundi Mil. 25
Tielemans mwenye umri wa miaka 20 ametia saini mkataba wa miaka mitano na Monaco akitokea Anderletch, mkataba utakaomfanya aitumikie hadi June 2022.
Monaco ambao ni mabingwa wapya wa Ufaransa wamefanikiwa kumnasa kiungo huyo pamoja na ushindani kutoka vilabu vikubwa kama Manchester United,Manchester City, Liverpool na AS Roma na Everton.
Awali mkurugenzi wa michezo wa Anderletch alisema kuwa Tielemans amesajiliwa kwa ada ya uamisho wa paundi mil.21 pamoja na marupurupu.
Makamu wa Rais wa klabu ya Monaco Vadim Vasilyev amesema kuwa, Youri amekuwa akiwindwa na vilabu vikubwa vya ulaya lakini mwenyewe ameichagua Monaco kwaajili ya maendeleo yake ya soka.
"Tunafurahi kwasababu kuja kwake kunadhihirisha kuwa mradi wetu unaongezeka mvuto. Kuwasili kwake ni mwendelezo wa mikakati yetu ya kusaka vijana wadogo wenye vipaji" Aliongeza Vadim.
Youri anasajiliwa na Monaco ikiwa ni mwendelezo wa mafanikio yake binafsi kwani ametoka kutajwa kuwa mchezaji bora wa ligi kuu ya Ubelgiji almaarufu Pro League
Youri Tielemans akiwania mpira na kiungo wa Manchester United Paul Pogba kwenye mechi ya Europa |
Comments
Post a Comment