AC Milan imefanikiwa kuinasa saini ya mlinzi wa Villareal Mateo Musacchio (26) kwa dau la Euro milioni 18.
Musacchio amesaini mkata wa miaka 4 na magwiji hao wa Italy utakaombakisha San Siro hadi mwaka 2021, baada ya kukamilisha vipimo vya afya wiki iliyopita.
Muargentina huyo mwenye umri wa miaka 26 alisainiwa na Villareal akitokea River Plate mwaka 2009 ambapo alianza kwa kuitumikia timu ya vijana, Villareal B na baadae kupandishwa timu ya wakubwa ambapo February 2, 2010 na alicheza kwa mara ya kwanza akiingia dakika 15 za mwisho dhidi ya Athletico Bilbao katika ushindi wa magoli 2-1.
Katika klabu ya Villareal, Musacchio ameichezea zaidi ya mechi 200 kabla ya kufikia makubaliano haya ya kuhamia San Siro.
Usajili wa mlinzi huyu unakuwa wa kwanza kwa AC Milan katika majira haya ya joto huku ikionekana dhahiri kuwa Milan wamepania kuboresha zaidi kikosi chao msimu ujao ili kurejea katika michuano ya Ligi ya mabingwa Ulaya.
Kwasasa Milan wamemaliza katika nafasi ya sita(6) katika msimamo wa Serie A pamoja na kuanza kwa kasi, na hivyo watashiriki michuano ya Europa mwakani.

Comments
Post a Comment