Michuano ya kombe la Africa kwa vijana wenye umri chini ya miaka 17 inafunguliwa rasmi leo huko nchini Gabon kwa michezo miwili.
Wenyeji wa michuano timu ya Gabon wanakabiliana na Guinea majira ya saa 9:30 jioni katika mchezo ambao nidhamu yake itasimamiwa na refa kutoka Kenya Davies Ogenche Omweno, hapo baadae saa 12:30 kutakuwa na mchezo wa pili kati ya Cameroon na Ghana.
Serengeti Boys wao wataanza kutupa karata yao kesho saa 9:30 jioni dhidi ya Mali huku msimamizi wa mchezo huo akiwa ni refa kutoka Nigeria Ferdinand Udoh Aniete.
Serengeti Boys watajitupa uwanjani huku wakiwa na recodi nzuri katika maandalizi kuelekea michuano hii. Walianza kwa ushindi mara mbili dhidi ya Burundi wa 3-0 na 2-0 kabla ya kudroo na Ghana. Pia waliwapiga waandaaji Gaboni kwa 2-1 na pia Morocco kwa goli 1-0.
RATIBA YA HATUA YA MAKUNDI (muda si majira ya Africa Mashariki)

Comments
Post a Comment