- Ni siku moja tu baada ya Moyes kutimuliwa sunderland
Big Sam amewashtua wengi kwa taarifa hiyo ikiwa ni siku chache tu tangu aisaidie kusalia katika ligi huku akifanya makubwa katika ungwe ya mwisho kwa kuvitandika vilabu vikubwa kama chelsea,Liverpool na Arsenal .
Sam ameeleza sababu zinazopelekea yeye kuchukua maamuzi haya kuwa ni kushindwa kukubaliana na uongozi wa klabu hiyo katika suala zima la usajili.
Allardyce alitaka kukutana na mwenyekiti Steve Parish kuhusiana na kuhakikishiwa kutimiziwa mikakati yake ya usajili wa dirisha kubwa kabla ya kukubaliana kukiona kwa muda zaidi kikosi hicho. Inasemekana kuwa moja wa vipaombele vya Big sam katika kuboresha kikosi ni pamoja na mlinzi Mammadou Sahko aliyekuwa hapo kwa mkopo na kuendelea kumbakisha Luka Milivojevic pamoja na kuongeza wengine.
Hivyo hatua hii kwa Sam ni kama kushindwa kuheshimu mawazo na malengo yake hivyo kutaka kuachana na timu hiyo.
Hali hii si ya mara ya kwanza kwa crystal palace kwani miaka mitatu nyuma, kocha Tony Pulis ambaye kwasasa anainoa West Brom aliachana na Palace kwa madai kama haya.
Big sam aliyekuwa kocha wa sunderland zamani akiichukua Palace baada ya kutupiwa virago katika timu ya taifa ya uingereza. Hata hivyo Sunderland ambayo imemtimua kocha wake David Moyes jana mashabiki wake wamekuwa wakishinikiza kurejeshwa kwa Sam allardyce.
Comments
Post a Comment