Shirikisho la mpira wa miguu duniani FIFA limethibitisha kuwa Africa sasa itapeleka timu 9 hadi 10 kushiriki katika michuano ya kombe la Dunia kuanzia mwaka 2026.
FIFA wamefikia maamuzi hayo katika mkutano uliofanyika Bahrain ikiwa ni mchakato wa kuongeza idadi ya timu shiriki kutoka 32 mpaka 48.
Africa yenye imekakikishiwa nafasi 9 za lazima katika michuano hiyo, huku nchi itakayoshika nafasi ya 10 kucheza mechi ya mtuano (play off) kugombania nafasi 2 za timu zitakazoongezwa kukamilisha idadi kamili ya timu 48.
Pamoja na habari hii ya matumaini kwa bara la Africa, kwingikeko bara la Amerika ya Kusini, kati na Kaskazini wanaonekana kunufaika zaidi na fursa hii.Bara la Amerika ya Kusini lenye nchi washiriki 10 wameongezewa idadi ya ushiriki kutoka 4 hadi 6 na atakayeshika nafasi ya 7 kucheza mtuano hivyo kufanya uwezekano wa kupeleka timu 7. Ulaya wameongezewa kutoka washiriki 13 hadi 16 wakati Amerika ya kati na kaskazini wakiongezewa mara mbili kutoka 3 hadi 6.
Kwa upande wa bara la Asia nao wameongezewa kutoka washiriki 4 hadi 8. Nchi za ukanda wa Bahari ambazo zilikuwa na nafasi ya 1 tu iliyokuwa inatumika kwenye mtuano, sasa imepata nafasi moja ya uhakika kushiriki kombe la dunia. Ikumbukwe pia kuwa Australia kwa sasa wameungana kisoka na shirikisho la AFC hivyo kucheza michuano ya kufuzu na timu za bara la Asia.
Kampeni hii ya kuongeza timu washiriki hadi kufikia 48 imekuwa ni kipaombele kikuu cha Rais wa sasa wa FIFA Gianni Infantino.
Na Walter Stephen.

Comments
Post a Comment