Skip to main content

Usajili wa Paul Pogba kwenda Manchester Utata mtupu, FIFA kuuchunguza

Usajili wa kiungo Mfaransa Paul Pogba uliovunja rekodi ya dunia mwaka jana akitokea Juventus kwenda Manchester United unatarajiwa  kuchunguzwa na Shirikisho la soka duniani FIFA.
Dili hilo lililohusisha kitita cha paundi milioni 89 limegubikwa na taarifa zinazokinzana na taratibu za usajili zinazomhusisha wakala wa mchezaji huyo Mino Raiola.

Raiola anashukiwa kwa kosa la kusimamia usajili huo kwa kufanya kazi hiyo kama mhusika upande wa wanunuzi, na kwa wakati huo huo akisimamia upande wa wauzaji na hivyo kumfanya awe amehusika kwa pande tatu za usajili huo kutokana na yeye kuwa tayari ni wakala wa Pogba. Kwa mujibu wa taratibu za FIFA jambo hilo halikubaliki isipokuwa kwa sababu maalumu ambazo zinatakiwa ziwafikie FIFA.
Taarifa hizo zimetolewa na kitabu kilichochapiswa nchini ujerumani chenye kichwa cha habari "The Dirty Business in Football" ikimaanishwa "Madudu yanayofanyika kwenye biashara ya Mpira" kinachoandikwa na waandishi wa habari wawili wa Ujerumani na hutoka kwa awamu.

Inasemekana kuwa katika usajili huo uliomfanya Raiola kunufaika kwa kufanya majukumu matatu ulimpelekea kukubaliana na Manchester United kulipwa kitita cha paundi milioni 41 huku sehemu ya fedha hiyo ikilipwa kwa awamu.

Mpaka sasa si Pogba wala Raiola aliyezungumzia sakata hilo, na waandishi walipomhoji Raiola, alisema swala lake linashughulikiwa na wakili wake na hivyo hayupo tayari kulitolea ufafanuzi wowote.

Kocha wa Machester Jose Mourinho amesema hii leo kuwa, sakata hilo halitamathiri Pogba kwa sasa ambaye yeye na wachezaji wenzake wanajifua kuwakabili Celta Vigo kukamilisha ungwe ya nusu fainali ya kombe la Europa
usiku majira ya saa 6 pale Old Trafford.

Pogba anaitumikia Manchester United kwa awamu ya pili sasa alisajiliwa kutoka Juventus baada ya awali kununuliwa na vibibi vizee hio vya Turin (Juventus) akitokea hapo hapo Old Trafford.
Kabla ya kuitumikia Manchester kwa mara ya kwanza, Pogba alisajiliwa kutoka klabu ya Le Harve inayoshiriki ligi daraja la pili Ufaransa yaani French League 2.

Comments

Popular posts from this blog

Wajue Wafungaji bora wa EPL kwa kila timu inayoshiriki sasa

1. CHELSEA - Frank Lampard -147 Lampard ndiye anayeshikilia rekodi ya mfungaji bora wa Chelsea wa muda wote yaani tangu (Chelsea) ilipoanzishwa akitupia kambani magoli 211. Alisajiliwa akitokea West ham mwaka 2001 na kwa sasa ni moja kati ya mashujaa wa kubwa wa klabu ya Chelsea. Alifunga goli la kwanza la Premier League akiwa na Chelsea December 23, 2001. Goli la mwisho alilifunga 05 April 2014. 2. TOTTENHAM - Teddy Sheringham - 98 Teddy Sheringham anafahamika kama "Legend" wa Tottenham Hotspurs pamoja na kuvichezea vilabu takribani 10 vya nchini uingereza ikiwemo Manchester United na West ham United. Alisajiliwa na Tottenham akitokea Nottingham Forest mwaka 1992 na alisajiliwa na Man United 1997 kabla ya kurejea tena Tottenham 2001. Aliifungia Spurs goli la kwanza tar.02.september 1992 na la mwisho tar. 21 April 2003 kabla hajatimkia Portsmouth   3. MANCHESTER CITY - Sergio Aguero -120 Akiwa amesaliwa na magoli 10 tu kuwa mfungaji bora wa historia wa M...

ABDULRAHMAN MUSA MCHEZAJI BORA WA MWEZI LIGI KUU

Mshambuliaji Abdulrahman Musa wa JKT Ruvu ameibuka mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom kwa mwezi April 2017 Katika kinyang'anyiro hicho Mussa amewapiku Jafar Salum wa Mtibwa Sugar na Zahoro Pazi wa Mbeya City. Si mara ya kwanza kwa Abdulrahman Mussa kupeba tuzo hii ya uchezaji bora wa mwezi. Katuika msimu wa 2015/2016 Mussa alitajwa tena kuwa mchezaji bora wa ligi kuu mwezi Mey 2016 huku akiwapiku wakali kama Donald Ngoma na Ali Nassoro ambapo alicheza michezo mitatu mwezi huo na kufunga magoli 4. Mchezaji wa JKT Ruvu, Abdulrahaman Mussa (kulia) akipambana na Mshambuliaji wa  Mtibwa Sugar, Mohamed Ibrahim

Chelsea Mabingwa Wapya EPL 2016/2017

Michy Batchuayi apeleka shangwe kwa wapenzi wa "The Blue". Alazimisha sherehe ianze mapema. Sasa kurejea Stamford Bridge, Watford wakiwapoke kwa makofi kama wafalme .  Chelsea wametawazwa rasmi kuwa mabingwa wapya wa Uingereza, England Premier League baada ya kujikusanyia pointi ambazo hakuna timu yoyote kwasasa inayoweza kuzifikia. Mbelgiji Michy Batchuay ndie aliyelazimisha Chelsea kupewa tiketi ya kuanza kusherekea ubingwa wao baada ya kuipatia chelsea bao pekee dk ya 82 akiteleza kumalizia pasi iliyoingizwa na  Cesar Azpilicueta katika mchezo ulioonekana kuwa mgumu sana. Batchuayi alitokea benji akichukua nafasi ya Pedro Rodriguez katika mabadiliko mawili ya utata yaliowashangaza mashabiki wa Chelsea ambapo Eden Hazard naye alitolewa na nafasi yake kuchukuliwa na Willian. Baada ya mabadiliko haya Chelsea walianza kushambuliwa lakini ukuta wao ukiongozwa na Cahil, Luiz na Azpilicueta uliweza kuimili vishindo vya wenyeji wao. Michy Batchuayi akifunga goli 1 na l...